Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-Monduli

MKUU wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta amemueleza Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward Balele kuwa Wilaya ya Monduli haijawai kupata hati chafu tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, hivyo amemtaka aendelee kusimamia vyema ili hati chafu isiwepo..

Kimanta ameyasema hayo alipokuwa akimkabidhi ofisi Mkuu huyo wa Wilaya katika ofisi za Wilaya ya Monduli na kisha kuzungumza na watumishi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya na halmashauri.Amemtaka Mkuu uyo wa Wilaya kuhakikisha hadhi ya Wilaya ya Monduli inabaki kama ilivyo.

“Nakukabidhi Wilaya hii ya Monduli na watumishi wote wakiwa katika hali nzuri na wewe hakikisha unaendelea kufanya nao kazi vizuri na kwa ushirikiano mkubwa,"amesema.Amesema watumishi wa Wilaya ya Monduli kwa ujumla ndio waliofanikisha mafanikio yake hadi kufikia nafasi hiyo ya mkuu wa Mkoa, hivyo amewashukuru kwa ushirikiano wao waliouwonesha na kuwataka waendelee hivyo hivyo hata kwa mkuu huyu mpya wa wilaya.

Amesema Kimanta ameacha alama kubwa na nzuri sana katika wilaya hiyo na kuaidi kuyaendeleza yale waliyoweza kujifunza kutoka kwake huku wakishirikiana na Mkuu mpya wa wilaya.Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amekabidhi ofisi yake ya zamani ya wilaya kwa mkuu mpya wa wilaya hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema wiki hii.

Akizungumza Mara baada ya kukabithiwa ofisi ACP Balele aliahidi kumpa ushirikiano Mkuu wa mkoa Arusha na pia Kuwapa ushirikiano watumishi wa idara zote.Tayari mkuu huyo wa Wilaya amenza kazi ikiwa pamoja na kwa Kuendelea kusikiliza Wananchi na kutatua changamoto zao wanaofika ofisini kwake.Pia amefanya ziara ndogo kwa kutembea Kituo cha Polisi Monduli na kuzungumza na maafisa wa polisi.

Mkuu wa wilaya Mpya wa Monduli ACP Edward Jotham Balele akiongea na Wakuu wa Idara, Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli, Wachungaji na watu mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa ofisi kutekeleza Majukumu yake ya Ukuu wa Wilaya ya Monduli kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Iddi Kimanta ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta akionesha moja ya zawadi alizopewa na Wana Monduli wakati alipoenda kumkabidhi ofisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...