Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

RAIS Dk.John Pombe Magufuli amewatania wananchi wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambao wengi ni watani zake kwamba licha  Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo kuwa hajaolewa lakini wao wamekuwa wakimuangalia tu wala hawamuoni na hiyo ndio shida ya Wazaramo.

Utani huo wa Rais Magufuli kwa wananchi wa Kisarawe ambao wengi wao ni kabila la Warazamo ambao yeye ni watani zake ameutoa leo Juni 28,2020 wakati anazungumza baada ya kuzindua mradi wa Maji Kisarawe ambao umegharimu Sh.bilioni 10.6 na sasa umemaliza tatizo la changamoto ya maji ya muda mrefu ndani ya wilaya hiyo ambayo ni kongwe zaidi na historia inaonesha ilianza mwaka 1907 sawa na Mji wa Nairobi na sasa ina miaka 113
 
Akizungumza wakati anatoa pongezi kwa viongozi mbalimbali kutokana na kazi kubwa wanazofanya katika kuwatumikia wananchi, Rais Magufuli akatumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambapo alisema tangu ameingia kwenye Wilaya hiyo pamoja na mambo mengine ya kusimamia maendeleo amekuwa mstari wa mbele kutokomeza Zero ambazo huko nyuma zilikuwa nyingi sana.

"Nawapongeza Mawaziri, nawapongeza wakuu wa mikoa, nawapongeza wakuu wa wilaya ka kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi katika kuleta maendeleo.Hata Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amefanya kazi nzuri sana ya kuondoa zero , palikuwa na zero nyingi hapa, ninachoshangaa watani zangu Wazaramo hajaolewa lakini mmeshindwa kumuoa mnamuangalia tu hapa.Ndio shida ya Wazaramo saa nyingine mnashindwa mambo, "amesema Rais Magufuli wakati anatoa utani huo.

Mbali na kutoa utani huo, Rais Magufulia ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina kuhusu miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa ndani ya Wilaya hiyo ikiwa pamoja na kupeleka mablioni ya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ya barabara, maji, afya , elimu , umeme pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

Pia Rais Magufuli ameelezea ukongwe wa Wilaya ya Kisarawe ambayo ilianza wakati mmoja na jiji la Naiorobi nchini Kenya na ndio maana alikuwa akiumizwa kuona wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya maji, na hivyo kuamua kutoa maelekezo kwa Wizara ya Maji kuhakikisa maji yanapatikana na hatimaye leo amezindua mradi wa maji Kisarawe ambao utsaididia sio tu ndani ya wilaya hiyo bali na maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa kukumbusha tu Mkuu wa wilaya ya Kisarawe baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa katika wilaya hiyo moja ya jambo ambalo amelisimama na kulipa kipaumbele ni kuhakikisha anaondosha zero katika shule mbalimbali za Wilaya ya Kisarawe ambazo zilikuwa nyingi.
Hivyo aliamua kuanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga shule ya wasichana na tayari shule hiyo ambayo imejengwa kata ya Kibuta imekamilika na kupewa jina lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...