Vero Ignatus.
Msongo wa mawazo kwa madereva wa safari ndefu ikiwemo malori na mabasi,kutokana najanga la covid-19 umetajwa kuwa chanzo cha ajali za barabarani.
Janga la Corona lililongia hapa nchini mapema mwezi wa tatu mwaka 2020,limevuruga halihaisi ya utendaji kazi,limepunguza uzalishaji hivyo madereva wengi kukosa muda wa kupumzika,hujawa na uchovu,kutokula mlo kamili,pamoja na uchovu wa kuendesha gari kwa muda mrefu,yote haya yana,unaosababisha kinga zao za mwili kushuka na kuwa mashakani kupata maabukizi ya ugonjwa wa Corona.
Abdulmajid Abdulazizi Mwasha ni dereva wa safari marefu kutoka Tanzania kwenda Rwanda, anasema kutokana na janga hilo lililoikumba dunia la Covid-19 , asilimia kubwa madereva wa malori wameathirika, hususani katika nchi wanazokwenda wamekuwa wakitengwa na kuonekana wao ndiyo chanzo cha maambukizi ya ugonjwa huo.
''Tunapoingia katika mipaka ya nchi za wenzetu, tunaonekana sisi ndiyo tunaopeleka ugonjwa wa Corona, kiasi kwamba ukivuka tu mpaka , huruhusiwi kusimama popote na hata ukipata breakdown hakuna wa kukusaidia,jambo la kushangaza zaidi ni kwamba askari wa nchi hizo, wanawatembelea nyumba zilizopo jirani na tunakofikia sisi na kuwaambia wasitusogelee kwasababu tuna corona, jambo hili limekuwa likituumiza sana kisaikolojia na kutusababishia msongo wa mawazo''.Anasema Abdulmajid Mwasha..
Alisema hali halisi ya unyanyapaa inawaumiza madereva,kila wanapofika nchi jirani na kuongeza kuwa japo,upo utaratibu kwa utaratibu uliowekwa wa kusindikizwa bado madereva wa masafa marefu na wanapitia mazingira magumu ya kukosa huduma za kijamii,ameongeza kuwa katika mipaka mingi ya nchi jirani madereva wa Kitanzania wamepewa jina la corona,wanadhaniwa kuwa ndio wenye corona na wanaisambaza katika nchi jirani.
Kuhusu masuala ya vipato vya madereva Bwana Mwasha amanaesema,kwenye kampuni yao walikuwa na uwezo wa kwenda hata safari tatu kwa mwezi, lakini kutokana na janga hilo kwa sasa hawawezi kufanya hivyo kwani wamejikuta wanaenda safari moja, jambo ambalo limewafanya athari ya kisaikolojia kuwa kubwa zaidi ikichangiwa na athari ya kusuka kwa kipato,kuathirika kisaikolojia,kiuchumi, pamoja na changamoto wanazokutana nazo kutokana na ugumu wa kazi yao, zinawapa msongo wa mawazo, kwa asilimia kubwa jambo ambalo linaweza kusababisha ajali wawapo safarini.
''Vipato vimeshuka,tunafamilia,hatuna muda wa kutosha kupumzika,hatupati mlo kamili,utendaji wakazi umekuwa tofauti,hata katika depot za mafuta kazi zimepungua, mzigo unakuwa mwingi na kutokana na changamoto za nchi tunazokwenda mipaka yao haifanyi kazi(mafuta hayatumiki mengi)hivyo kwa njia moja hadi nyingine madereva wa malori ni wahanga wakubwa wa janga hili la''.Anasema Abdulmajid Mwasha.
Mmoja wa madereva kutoka chama cha madereva wa coaster(VTA) za kukodisha Jijini Dodoma(Kibasi Kiselekela siyo jina lake halisi) anasema kuwa karibu asilimia 90% ya madeva hawakuweza kufanya kazi kutokana na janga hilo la covid-19,matokeo yake wamekuwa wakienda kijiweni na wanarudi nyumbani bila kupata chochote na malipo ya kazi yao yanapatikana mara dereva anapokwenda safari.
''Unamkuta dereva amebahatika kupata kazi moja kwa mwezi mzima,ana familia watoto nyumbani wanahitaji kula,anadaiwa kodi ya nyumba,bado ana mahitaji binafsi hivi kweli ataacha kusababisha ajali kweli ukizingatia hii kazi haina mashahara unajilipa kutokana na kazi unayoipata''.Alihoji Kibasi Kiselekela
Nassor Mansour Nassor ni mmiliki wa vyombo vya usafiri Mtwara -Lindi pamoja na wilaya zake,anasema athari katika sekta za usafirishaji baada ya kutokea janga la covid 19,limewaathiri kwa kiasi kikubwa,hususani wamiliki walioingia kwenye mikopo benki pamoja na wale walioingia mikopo na watengenezaji wa magari hayo (mabasi ya abiria) haswa mabasi makubwa yanayofanya safari ndefu
Mansour anasema kuwa maelekezo ya serikali, kuwataka watu kukaa mbalimbali na kupunguza mikusanyiko wa abiria kwenye magari ya umma ili kuzuia kusambaa virusi vya corona, kumethri kipato katika sekta ya usafirishaji,na hivyo kulazimika wamiliki wengi wamelazimika kupunguza na wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji au kusitisha shuguli zao kwa kuhofia kupata hasara.
''Abiria nao walipungua kwakuwa watu wengi walisitisha safari, sababu walifuata maelekezo ya wataalam wa afya pamoja na serikali kujikinga na maambukizi, hivyo magari mengi pia hayakuweza kufanya kazi ,pamoja na wamiliki, madereva pia wameathrika sana''.Anasema Nassor Mansour
Ameeleza kuwa athari kubwa iliyopatikana ni kutokupatikana kwa kile kipato cha kila siku kilichokuwa kinategemewa,mfano ulikuwa na gari ndogo ambayo labda ulikuwa unategemea upate labda elfu 80,000-100,000 ilifikia hatua gari linakwenda kazini hata siku tatu hawapati chochote zaidi ya hasara.
Siyo hivyo tu kuna wale waliochukua mikopo benki wameshindwa kufanya marejesho ya benki, lakini pia kuna wale walioingia mikopo au mikataba ya kukopeshana magari na wenye makampuni ya China yanayotengeneza hayo magari nayo pia athari yake imekuwa kubwa sana kwasababu wameshindwa kutimiza lile lengo lililokuwa linahitajika kwa kulipa mikopo kwa wakati.
Kwa kanda yetu hii ya Mtwara wapo wamiliki wana mabasi 15-16 ,siku ilikuwa tunatoa basi siyo chini ya 20 lakini ilifikia hatua kwa siku tulikuwa tunatoa basi mbili,mmiliki huyu anapataje kipato cha kurudisha rejesho?! wengi wamefikia hatua ya kuuza vitu vyao ambavyo hawajawaweka rehani benki,ikiwemo nyumba,na baadhi ya magari,wengi wanauza magari kwa bei chee kwasababu ya athari ya gonjwa hili la covid-19.Alisema Nassor
Kwa upande wa daladala anasema hata lile agizo lililotolewa na serikali la abiria kutojazana kwenye mabasi (level sit) kwa mikoani suala hilo lilijitengeneza lenyewe siyo kwamba askari walitumia nguvu nyingi la hasha! kwani abiria walikuwa wachache,hivyo kusababisha gari kusafiri kwa hasara bila faida
Athari nyingine abiria kuwa wachache hadi kukosa safari za mara kwa mara hivyo maisha ya madereva yalikuwa magumu kwani watu waliokuwa na changamoto kubwa ni madereva wa mabasi ya abiria,kwani nikama vile tulijitoa muhanga kipindi ambacho ugonjwa ukiwa umepamba moto,ila tunamshukuru Mungu ugonjwa umepungua na tuendelee kuomba uishe kabisa.Anasema Jabu Daruweshi Chegenya
Kwakweli malipo ya posho yamepungua sana wakati mwingine kukosa kupewa kabisa na ukianagalia kweli habiria hakuna na waliopo ndani ya gari hata malipo ya mafuta kutoka mwanza kuja Dar es salaam ni changamoto kubwa na tajiri mwenyewe haimlipi ,hivyo changamoto za kiuchumi mapato zinasababisha msongo mkubwa wa mawazo kwa madereva wengi. Anasema dereva wa bus la abiria Jabu Daruweshi Chegenya
Ugonjwa huu wa covid-19 ulituathiri sisi madereva kwanza kiasi kikubwa,kilichokuwa kinatupa hofu kubwa ya kuambukizwa ni pale serikali haikuweza kusitisha shughuli za usafirishaji wa abiria nchini,hivyo hofu ya kuambikizwa ilikuwa kubwa sana kwetu madereva
Hivi karibuni chama wamiliki wa malori nchini (TATOA) kupitia mwenyekiti wake Elias Lukumay waliiomba serikali kuketi na pamoja katika mazungumzo na viongozi wa nchi jirani ili kutatua changamoto ya madereva wa malori kutokana na hali ya kunyanyasika mipakani kwenye katika kipindi cha ugonjwa wa mapafu wa covid-19 na kuangalia hali wanazopitia madereva hao.
Lukumay aliweza kuainisha changamoto ambazo wanakabiliana nazo madereva hao ni pamoja na unyanyasaji unaofanyika,unyanyapaa unaofanyika mpaka Rusumo unaounganisha Tanzania na Rwanda ,pamoja na ule wa Namanga wanapotaka kuvuka kuingia nchini Kenya, licha ya kuwepo makubaliano yaliyofikiwa lakini kuna mambo yanaendelea kujitokeza,pamoja na madereva kukaa kwa muda mrefu katika eneo la Gaina ambalo halina huduma toshelezi kwa jamii .
Pia suala la kukaa kwa muda mrefu kumesababisha hasara kwa wafanyabiashara ,pamoja na wasafirisaji wa Tanzania kuendelea kutozwa faini kiasi cha 120,000 kwa siku,huku madereva wakiishiwa pesa za kujikimu baada ya kukaa kwa muda mrefu

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...