Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Geita
Josephat Maganga kuelekea kuzungumza na watendaji wa sekta ya ardhi
katika mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta
ya ardhi mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa
sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kukagua utendaji
kazi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Geita Josephat Maganga na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa
Geita Rugambwa Banyikila

Baadhi ya Watendaji wa sekta ya
ardhi katika mkoa wa Geita awakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiingia kukagua jengo la Ofisi
ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Biharamulo mkoa wa Geita
lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati wa ziara yake
katika mkoa wa Geita mwishoni mwa wiki.

Taswira ya jengo la Ofisi ya
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Biharamulo mkoa wa Geita lililojengwa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa wilaya ya Chato, Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu na
watendaji wengine mbele ya jengo la Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)
Biharamulo mkoa wa Geita wakati wa ziara yake katika mkoa ho mwishoni
mwa wiki. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Munir Shemwta, WANMM GEITA
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka
halmashauri nchini kupitia idara zake za ardhi kuhakikisha zinapima
maeneo yote yenye migodi ili kuondokana na migogoro.
Dkt Mabula
alisema hayo mwishoni mwa wiki aipozungumza na watendaji wa sekta ya
ardhi kwenye mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kukagua utendaji wa
sekta ya ardhi pamoja na utekelezaji wa miradi inayofanywa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) mkoa humo.
Dkt Mabula
alisema, mkoa wa Geita una migodi mingi bila kuwa na suala la upimaji na
umilikishaji maeneo ya Migodi migogoro kwenye maeneo hayo haitaisha kwa
kuwa leseni ya uendeshaji shughuli za uchimbaji madini inaonesha
umiliki eneo la chini lenye madini.
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitolea mfano wa Mgodi wa Madini wa
Nyamongo kuwa, umefanikiwa kupima maeneo yake na sasa mgodi huo pamoja
na kuwa na haki ya umiliki eneo la chini la madini (mineral rights)
lakini Mgodi huo inamiliki pia eneo la juu (surface rights) na hivyo
kuondokana na migogoro.
‘’Hakikisheni
wanaoendesha shughuli za migodi wanamiliki kihalali maeneo yao, ana
surface rights na ana minerals rights ili awe salama habari ya
kufukuzana na watu wanaopita juu haipendezi, ana haki ya kuwa pale juu
kwa sababu wewe leseni yako ni ya kule chini sasa wewe unaniondoaje’’
alisema dkt mabula
Kwa mujibu wa Dkt
Mabula, kwa bahati nzuri kwa sasa wachimbaji wadogo nao tayari wameanza
kuanishiwa maeneo hivyo kasi ya kuyapima maeneo hayo iongezeke ili
wanaoendesha shughuli za migodi wamiliki kihalali maeneo yao sambamba na
kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi ya ardhi kwa serikali.
Amewataka
watendaji wa sekta ya ardhi katika maeneo yenye migodi kuangalia namna
bora ya kuzungumza na wamiliki hao ili kutambua umuhimu na faida ya
kupima maeneo yao kwa lengo la kuondokana na mgogoro.
Akiwa katika
wilaya ya Chato ambako alikagua pia mradi wa ujenzi wa ofisi ya Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Biharamulo unaofanywa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC), Dkt Mabula ameitaka wilaya hiyo kuandaa mpango wa
mji huo ili kuwa na sura ya kitalii na kusisitiza utolewaji elimu kwa
viongozi wa vijiji kuwaelekeza wananchi umuhimu wa kujenga nyumba kwa
mpangilio ili kuepuka ujenzi holela
Naibu Waziri
Mabula aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Chato
kufuatilia wananchi wasijenge kiholela na kubainisha kuwa NHC inaweza
kutumika katika kupanga miji kupitia ujenzi wa nyumba zake ili kuzuia
ujenzi holela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...