Na Leandra Gabriel, 
Michuzi TV
BIASHARA ya utumwa nchini Ireland ilianza kwa binadamu kuuzwa, wakati wa utawala wa Mfalme James wa pili aliporuhusu kuuzwa kwa wafungwa 30,000 wakiwemo wanaume, wanawake na mabinti wadogo.

Katika miaka ya 1660 Ireland ilikua kitovu cha biashara ya utumwa na wengi wao waliuzwa katika maeneo ya Antigua na Montserrat na kwa wakati huo asilimia 70 ya watu Montserrat walikuwa watumwa kutoka Irish.

Ireland  imeandikwa katika historia kwa kuwa kitovu  cha biashara ya wanadamu kwa wafanyabishara wa kiingereza, na hadi sasa raia wengi wa nchi hiyo wanaishi nje ya nchi ukilinganisha na wanaoishi ndani ya nchi.

Historia inaonesha kuwa katika miaka ya 1641 hadi 1652 zaidi ya raia 500,000 kutoka Ireland  waliuwawa wakiwa utumwani huku wengine 30,000 wakiuzwa hali iliyopelekea kupungua kwa idadi ya watu nchini Ireland kutoka 1,500,000 hadi kufikia 600,000 kwa muongo mmoja, wanawake na watoto waliachwa wakitangatanga wakiwa na changamoto za kimaisha kwa kuwa waingereza hawakuwaruhusu kubeba familia zao.

Imeelezwa kuwa katika miaka ya 1650 zaidi ya watoto 100,000 wa Irish wenye miaka 10 hadi 14 walichukuliwa kutoka kwa wazazi wao na kuuzwa katika mataifa ya India na Uingereza na mwaka 1656 wakati wa utawala wa Cromwell alitoa agizo la kuuzwa kwa watoto 2000 waliouzwa nchini Jamaica, na hadi kufikia mwaka 1798 Uingereza iliendelea kuwatumia watumwa kutoka Irish na watumwa wengine walipelekwa katika mataifa ya Amerika na Australia.

Wafanyabiashara wa utumwa walianzisha mahusiano na wanawake wa Irish lakini bado watoto wao wakabaki watumwa na hawakuwa na uhuru na hata walipowazalisha watoto waliandaliwa kuwa watumwa.

Katika karne ya 17 na 18 watumwa kutoka Irish walishuka thamani walichukuliwa kama wanyama na katika wakati huo biashara ya utumwa ilianza Afrika lakini ilipewa thamani sana.

Watumwa kutoka Afrika walikuwa ghali ukilinganisha na watumwa kutoka Ireland ambao waliuwawa na halikuwa kosa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...