WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amevitaka vyuo vyote nchini kuhakikisha hadi kufikia ijumaa Juni 5, mwaka huu viwe vimeshawalipa wanafunzi wote fedha zao za kujikimu na ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo Juni 3, 2020  jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi magari manne kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho  ni miongoni mwa vyuo vinne vitakavyonufaika na mkopo huo wa Benki ya Dunia kupitia mradi wao wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP).

Profesa Ndalichako amesema kuwa kuna baadhi ya vyuo mpaka leo bado havijawapatia wanafunzi fedha hizo za kujikimu licha ya kwamba Serikali imeshazitoa hivyo anatoa siku tatu kuanzia leo kuhakikisha wanazitoa ili wanafunzi waendelee na masomo bila kupata usumbufu wowote.

"Wanafunzi ikifika Ijumaa ya wiki hii mume mmeshalipwa fedha zenu na chuo ambacho hakitafanya hivyo hakuna msalia mtume,  wizara yangu haitaweza kukivumilia kwa sababu hakuna sababu ya kuchelewesha kufanya malipo hayo kwa kuwa fedha tayari zilishapelekwa vyuoni," amesema Ndalichako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...