Na Ashura Mohamed -Arusha

Tume ya taifa  ya  Uchaguzi (NEC) kupitia Ofisi ya Afisa Mwandikishaji  ambae ni  Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Jiji la Arusha imesema kuwa itaweka wazi Daftari la Awali la  Wapiga Kura kwa siku nne mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa  habari  jijini Arusha pamoja na wawakilishi wa Vyama vya Siasa mkoani Arusha,Afisa Uandikishaji  Msaidizi  wa Jiji hilo,Misena Bina,alisema  daftari litakuwa wazi kuanzia  June 17-20, katika vituo vilivyotumika awali wakati  wa Uboreshaji  wa  Daftari la  Kudumu  la Wapiga Kura.

Alisema kuwa Wakati wa zoezi hilo la uwekaji wazi
Daftari la Awali la  Wapiga Kura litafanyika kwa kuzingatia  tahadhari  zote  za Afya kuhusu kuzuia maambukizi  ya Ugonjwa wa Covid-19,unaosababishwa na Virusi vya Corona.

"Wahusika ni Wapiga Kura wote walioandikishwa katika daftari la kudumu,la wapiga Kura mwaka 2015,walioandikishwa wakati wa Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Awamu ya kwanza na ya Pili kwa mwaka 2019/2020"alisema bwana Bina.

"Wapiga kura Hawa ni wale ambao hawakuhakiki taarifa zao, wakati wa uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura Awamu ya kwanza,Wapiga Kura watakaohakiki taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura lolipowekwa wazi na kukuta picha zao hazipo mwanatakiwa kwenda shule ya msingi Meru,karibu na kituo Cha Afya Kaloleni ili wapigwe picha nyingine haraka"alisema bwana  Bina.

Hata hivyo alisema kuwa Mambo ya kuzingatia ni Daftari la Awali la Wapiga kura litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha Wapiga kura.

Nae  Afisa  Uchaguzi  wa Jiji la Arusha bi.Namyaki Naitetei alisema kuwa Pingamizi zote zitawekwa kwa vielelezo na ushahidi na sio maneno matupu.

Pia aliwataka Wapiga kura kutoa taarifa za ndugu waliofariki dunia ili waondolewe kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.

"Nataka niwaambie zoezi hili  hakutakuwa na uandikishaji wa Wapiga kura wapya,Aidha hakutakuwa na Uboreshaji wa taarifa za Wapiga kura waliohama maeneo ya kiuchaguzi waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika"alisema bi.Namnyaki.

Bi.Namnyaki aliwataka wakazi wa Jiji la Arusha kuzingatia kanuni za Afya kwa kufuata maelekezo watakayopewa wawapo vituoni,ili kujiepusha na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...