Jumla ya Nyavu 110, kokoro 2 na timber 32 zilizokuwa zinatumika katika uvuvi haram zimekamatwa na kuteketezwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Vifaa hivyo vimekamatwa kati ya tarehe 19/05/2020 na 04/06/2020 katika vijiji vya Nyakaboja kata ya Kabita na Maega Kata ya Kalemela.

Uvuvi haram umekuwa changamoto ukanda wa Ziwa Viktoria, hivyo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Busega imeanza kupambana na wavuvi wanaotumia vifaa visivyokubalika kwenye shughuli za uvuvi ili kuzuia uharibifu wa rasimilimali kwenye Ziwa Viktoria.

Kwa upande mwingine Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imewataka wavuvi wote wilayani humo kufuata sheria za uvuvi kwa kufanya shughuli zao za uvuvi kwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali, kwani uvuvi haram umekuwa moja ya changamoto kwenye ukusanyaji wa mapato yanayotokana na shughuli za uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...