*Pia kurejesha shughuli zote zilizosimama...asema maisha lazima sasa yaendelee
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS Dk.John Magufuli ametangaza rasmi kuwa Juni 29,2020 shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa kwasababu ya janga la Corona zifunguliwe huku akitumia nafasi hiyo pia kutangaza kurejesha shughuli zote za kijamii na kimaendeleo ambazo nazo zilisimama.
Ametoa kauli hiyo leo Juni 16,2020 Bungeni Mjini Dodoma wakati akitoa hotuba ya kuvunja Bunge la 11 ambalo limemaliza muda wake rasmi leo, hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza wazi kuwa kwa sasa nchini Tanzania maambukizi ya Corona yamepungua sana na hivyo shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa zifuguliwe rasmi Juni 29 mwaka huu.
"Juni 29,2020 shule zote ambazo zilikuwa zimefungwa kwasababu ya Corona zifunguliwe. Pia shughuli zote ambazo zilikuwa zimesimama kupisha janga hilo nazo tunaruhusu zianze kuanzia tarehe hiyo, maisha lazima yaendelee.Nawashukuru Watanzania wote kwa kushinda vita dhidi ya mapambano ya Corona,"amesema Rais Magufuli.
Akizungumzia janga la Corona , Rais Magufuli amesema kuwa Serikali yake iliamua kupambana na janga hilo kikamilifu huku akifafanua matatizo au changamoto hazikimbikiwi kwani kukimbia changamoto ni ishara ya udhaifu, ni ishara wa woga ni ishara ya kutojiamini.
"Siku zote njia ya kukabiliana na changamoto ni kukabiliana nayo, ndio maana tuliamua kukabiliana na Corona kwa kumtanguliza Mungu na mpaka sasa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Sio tu kufanikiwa kuushinda ugonjwa huo bali pia kushinda athari zake iwemo ya kiuchumi.
"IMF ilitoa taarifa kuwa nchi za Kusini mwa Afrika na asilimia ya 60 ya nchi za Afrika uchumi wake utashuka kutokana na janga la Corona, lakini kwa hatua ambazo tumechukua uchumi utakuwa hautashuka bali utaendelea kukua kwa asiilimia tano hivi.
"Tumelinda ajira za watu wetu, na hivyo inaonesha maamuzi yetu yalikuwa sahihi na hata Bunge kuendelea na vikao nako kulikuwa ni uamuzi sahihi sana, hongera Spika wa Bunge, hongereni wabunge.
"Kwa hiyo nitumie fursa hii kurudia kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na Corona lakini pia tunawashukuru viongozi weetu wa dini kuitikia mwito wa Serikali wa kufanya maombi.Najua kwenye Mungu hakuna kinachoshindakana,"amesema Rais Magufuli.
Pia emewapongeza madaktari kwa kazi nzuri, amewapongeza Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa ujasiri mkubwa ambao ameounoesha wakati wa janga la Corona.
"Nataka kusema kwa dhati nimtesa mama huyu, nilikuwa nampiga simu hadi saa nane usiku.Naomba aniombee msamaha kwa mumewe.
Namshukuru Waziri Mkuu na Kamati yake, nawashukuru Kamati ya Ulinzi na Usalama, nawashukuru Watanzania kwa kumtanguliza Mungu.
"Kwa hali ya Corona kuendelea vizuri na kweli imepungua sana.Juni 29,2020 mwaka huu shule zote zifunguliwe. Shule zote naziruhusu rasmi na maisha mengine lazima yaendelee,"amesema Rais Magufuli.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...