Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHANGWW zatawala bungeni Rais Magufuli akivunja Bunge! Hivyo ndivyo ilvyokuwa leo Juni 16,2020 ambapo nderemo, shangwe, vifijo vilivyoambatana na kila aina ya furaha vilitawala kwa wabunge wakati Rais Dk.John Maguli akitoa hutuba ya kuvunja rasmi Bunge la 11.

Wakati Rais Magufuli akiwa katika Bunge hilo ambalo limehimitisha majukumu yake na kutoa nafasi sasa ya kuanza rasmi kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, pamoja na mambo mengine, ametumia nafasi hiyo kueleza maendeleo na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali anayoiongoza lakini mafanikio hayo yametokana na mchango mkubwa na ushirikiano wa Bunge.

Rais Magufuli amewaambia wabunge kuwa kwa pamoja wamefanya kazi kubwa na nzuri na hakika wabunge na Bunge hilo la 11 wameandika historia ambayo itakumbukwa sasa na vizazi vijavyo kutokana na mchango wao mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu.

Hata hivyo baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja rasmi Bunge hilo la 11, wabunge walianza kupiga makofi yaliyoambatana na kila aina ya shangwe.

Baada ya Rais Magufuli kuketi kwenye kiti chake, ndipo aliposimama Spika wa Bunge Job Ndugai na kisha kutoa shukrani kwa Rais Magufuli kwa kazi kubwa ambayo ameifanya ya kulitumikia Taifa letu.

 Spika wa Bunge wakati anaendelea kuzungumza akafika katika eneo la kuzungumzia utaratibu kwa ajili ya wabunge hao ambapo aliwaaambia wabunge kuwa ombi lao kwa Rais Magufuli kwa ajili ya kuhusu utaratibu alilifikisha.

"Baada ya Rais kuvunja Bunge sasa, ile safari yetu ndio imefika mwisho wake leo, lakini tunafahamu mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa safari nyingine.

"Kuhusu utaratibu , nawashukuru Rais mbele yenu na hata hapo mlipokaa utaratibu unaendelea na utaratibu ni mzuri sana safari hii,"amesema Spika wa Bunge na hapo ndipo shangwe zilipochukua nafasi kwa wabunge kupiga meza na kilele.Mmoja ya wabunge alisikika akisema hivi "Magufuli Baba lao....Magufuli Baba lao...Magufuli Baba lao."

Itoshe tu wakati Rais Magufuli anavunja Bunge hilo wabunge walikuwa na shangwe na wale ambao walionekana kutopiga makofi na kushangalia Spika wa Bunge alisikika akisema hivi Asiyepiga makofi huyo atakuwa mchawi".

Hakika ilikuwa ni raha ya aina yake wakati wa kuvunjwa kwa Bunge hilo la 11.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...