Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli
amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu kuwa Brigedia Jenerali na wengine kuwa Meja
Jenerali kuanzia tarehe 02 Juni, 2020.
Miongoni
mwa waliopandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kanali (Balozi) Wilbert Augustin Ibuge na Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira
na wenye Ulemavu Kanali Francis Ronald
Mbindi.
Waliopandishwa cheo kuwa Meja Jenerali ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Kamishna Jenerali wa Magereza Brigedia Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Brigedia Jenerali Gabriel Saul Mhidze na Mkuu wa Chuo cha Maafisa Monduli Brigedia Jenerali Ibrahim Michael Mhona.
Imetolewa na
Luteni Kanali Gaudentius G. Ilonda
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano
+255754-635-412
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...