Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Dkt John Pombe Magufuli amezindua mradi wa maji  wa Kibamba Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Mradi huo umejengwa  kufuatia agizo alilotoa Juni 21,2017 wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa Ruvu Juu akiwataka Dawasa kutanua mtandao wa Usambazaji maji na kupeleka maji Kisarawe.

Akitoa maelezo ya mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Kisarawe umejengwa kwa fedha za ndani Bilion 10.6  zinazotokana na makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji.

Luhemeja amesema wakati wa utekelezaji wa mradi huo, Dawasa iliona fursa ya kujenga mradi mwingine wa Bilionj 7.3  wa kuyatoa maji katika tenki la Kisarawe linalohifadhi maji Lita Milioni 6  kupeleka katika maeneo ya Dar es Salaam.

Amesema, kukamilika kwa mradi wa maji Kisarawe  umewezesha maunganisho mapya  yapatayo 1650  na bado wanaendelea kufanya maunganisho mapya  na wananchi wanaendelea kupata maji safi.

Aidha, maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Kata za Kisarawe, Kazimzumbwi, Kiluvya, Kwembe, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya Viwanda.

Akizungumzia upatikanaji wa hali ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, Luhemeja amesema kwa sasa asilimia 88 wanapata maji kutoka asilimia 68 mwaka 2015 kwahiyo ni ongezeko kubwa la maji.

Pia lengo la Dawasa ni kuona kufikia mwaka 2025, asilimia 95 wanapata maji safi katika muda wote.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Dkt John Pombe Magufuli amezindua mradi wa maji  wa Kibamba Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...