Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo, wakati
wa kikao cha Kamati za Kudumu za Bunge za Masuala ya UKIMWI na Huduma za
Maendeleo ya Jamii kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa makubaliano ya
kimataifa ya afua za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

Wajumbe wa Kamati za Kudumu za
Bunge za Masuala ya UKIMWI na Huduma za Maendeleo ya Jamii wakisikiliza
taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa ya afua
za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU kutoka kwa Waziri wa Afya.

Mkuu wa Kitengo cha Kinga Mpango
wa taifa wa kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Magreth Kagashe akijibu swali lililoulizwa
mjumbe wakati wa kikao cha kamati ya kudumu za Bunge za Masuala ya
UKIMWI na Huduma za Maendeleo ya Jamii.

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu za
Bunge za Masuala ya UKIMWI na Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Oscar
Rwegasira Mukasa akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu mafanikio ya
utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa ya afua za kinga dhidi ya
maambukizi ya VVU iliyosomwa na Waziri wa Afya.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi
akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya Kudumu za Bunge za
Masuala ya UKIMWI na Huduma za Maendeleo ya Jamii.
******************************
Na WAMJW-DOM.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutekeleza makubaliano ya kitaifa na kimataifa juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini kwa kuweka mipango inayolenga kuzuia maambukizi mapya na kutoa huduma za tiba na matunzo kwa wanaoishi na VVU.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika kikao cha Kamati za Kudumu za Bunge za Masuala ya UKIMWI na Huduma za Maendeleo ya Jamii kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa ya afua za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU, katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau tumekuwa na mwitikio wa pamoja katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini kwa kuweka Mipango ya Kitaifa ambayo imekuwa ikilenga katika kuzuia maambukizi mapya na kutoa huduma za tiba na matunzo kwa wanaoishi na VVU” alisema.
Aliweka wazi kuwa, baadhi ya malengo yaliyotolewa ni Pamoja na, kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030, huku akisisitiza lengo kuu ni kuhakikisha uwepo wa uwajibikaji katika utoaji wa huduma bora za kinga dhidi ya VVU.
Aliendelea kusema kuwa, makubaliano haya yalianzishwa mwaka 2017 na nchi wanachama wa umoja wa mataifa, wahisani, asasi za kiraia na wadau mbali yakihusisha nchi 25 zenye viwango vikubwa vya maambukizi ya VVU ikiwemo Tanzania.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa, Utekelezaji wa makubaliano haya umekuwa ukipimwa kuanzia 2018 kupitia kadi maalumu ambayo inaonyesha taarifa muhimu za mwenendo wa utekelezaji wa malengo ya kitaifa yaliyowekwa na n chi kama vile huduma jumuishi za kinga kwa vijana rikabalehe na wanawake vijana (miaka 15-24) pamoja na wenzi wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...