Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

KIKOSI cha wachezaji wa timu ya Yanga pamoja a viongozi wao leo Juni 15,2020 wametinga Bungeni ambapo shagwe ziliibuka wakati wakisalimia huku Spika Job Ndugai akiuliza alipo mshambuli mahiri wa timu hiyo Benard Morrison.

Morrison ni yule mchezaji ambaye amejizolea umaarufu tangu alipofanikisha kufunga bao moja dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo Yanga waliibuka na ushindi.Juzi wakati Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alimtaja wakati akiwasilisha bungeni bajeti kuu ya Serikali.Hali ambayo ilisababisha shangwe kubwa bungeni.

Hata hivyo leo kikosi hicho kimeingia Bungeni bila uwepo wa mshambuliaji huyo ambaye bao lake dhidi ya Simba Waziri wa Fedha analifananisha na mkuki wa sumu.

Wakati anawatambulisha wachezaji hao wa Yanga ,Spika Job Ndugai alisikika akiuliza mahali alipo baada ya kutomuona bungeni wakati wachezaji wengine wakiwa ukumbini humo.

Mchezaji huyo mbali ya kutoonekana leo bungeni, pia hata katika mchezo wao wa juzi dhidi ya Mwadui FC Morrison hakuwepo uwanjani.Pamoja na kutoonekana kwa mchezaji huyo uongozi wa Klabu ya Yanga bado haujasema chochote.Yanga iliwasili Dodoma jana jioni na leo wameenda Bungeni.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...