Mwanasheria wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (Wildaf) Zakia Msangi akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya wiki Wajane Duniani namna Sheria zinazofanya kukosa haki Wajane hao.
Mkurugenzi wa Chama Cha Wajane Rose Sarwatt akizungumza na kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya Wajane na hatua mbalimbali za kuhakikisha wanapata haki na masuala mbalimbali katika jamii
Mjane Faith Mwankonsye -Okoyo akizungumza kuhusiana na changamoto za Wajane wanazokutanazo katika masuala ya mirathi.
Mkurugenzi wa Gender and Idolences Intiative (GIA) Idd Mziray akizungumza kuhusiana na mradi wa kuweza kutumia takwimu katika masuala ya waathirika wa Sheria.
-Wanawake wajane hawajui hata namna ya kufungua shauri la mirathi
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WilDAF) limesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia marekebisho ya sheria mirathi ili kuweza kutoa haki kwa wajane pindi wanapokuwa wamefungua shauri linalohusiana na mirathi.
Akizungumza na michuzi Blog kuelekea kilele cha siku wajane Duniani Mwanasheria wa Sherika hilo Zakia Msangi amesema kuwa serikali imekuwa karibu katika kuhakikisha maboresho ya sheria ya mirathi kwa wajane inaboreshwa na kazi hiyo wameendelea kuifanya kuweza kupata maboresho hayo.
Amesema kumekuwa na majadiliano ya wadau mbalimbali wanaoagazia masuala ya sheria ya wajane ,watoto ambapo serikali imekuwa ikishiriki kwa kuchukua mawazo katika kuweza kufanya maboresho ya sheria hizo.
“Tumeona dhamira ya serikali katika kufanyia marekebisho sheria ya mirathi hii itatoa haki kwa wajane ambapo ni tofauti na ilivyo kwa sasa kwani wajane wengi hawajui hata namna ya kuweza kufungua shauri la mirathi katika mahakama”amesema Msangi.
Ameongeza katika maboresho juu kuwepo kwa adhabu ya wafujaji mali za marehmu ili kuweza kuwa fundisho kwa wengine wanaokimbilia mali huku wakiacha wajane wakiteseka.
Nae Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Rose Sarwatt amesema katika maadhimisho hayo kufanya ni mara sita na kuwa na mwitikio mkubwa wanawake wajane katika kufikisha kilio chao katika masuala yanayowazunguka.
Amesema kuwa wana ofisi katika kila kanda ambapo wajane wengi wamekuwa na changamoto katika mirathi kutokana na mila na desturi ya wanawake kutopewa kipaombele pindi anapoondokewa na mwenza wake.
Mjane Faith Mwansye-Okoyo amaesema amesema wajane wanapitia katika changamoto kubwa pindi ndugu wa marehemu wanapofika katika kuhakikisha wanamiliki mali bila kujua hata mahitaji ya watoto.
Amesema kuwa katika suala muhimu ni kuwa na Utamaduni wa kuandika wosia kwa pande zote hali ambayo itapunguza dhuruma za mali za marehemu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...