Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema ndani ya miaka mitano chini ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli imepata maendeleo makubwa sana.
Ndikilo amesema, toka kupata kwa Uhuru mji wa Kisarawe haujawahi kupata maji safi na kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wamefanikisha kukamilika kwa mradi huo.
Mradi wa maji wa Kisarawe umeuzindulia leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli, tunafurahi sana kwa maji kupatikana ndani ya mji huu na pia kuna miradi mingi ya maji ndani ya mkoa wa Pwani.
Ndikilo, amesema Mkoa wa Pwani umefanikiwa kukusanya mapato ya Shilingi Bilion 53 ikiwa ni ongezeko kubwa katika kipindi cha miaka mitano.
Amesema, toka kuingia serikali ya awamu ya tano imeleta maendeleo makubwa, ikijenga Hospitali za Wilaya katika halmashauri zote tisa.
Mbali na hilo, Ndikilo ameeleza kuwa awali Mkoa wa Pwani ulikua unategemea kilimo cha Korosho na Ufuta ila kwa sasa wameongeza zao la Katani na kilimo cha miwa sambamba na kuanzisha kiwanda kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari.
Pia, Mkoa wa Pwani umepiga hatua kwa viwanda mbalimbali kuanzishwa ikiwemo Kiwanda cha nyama cha Tanchoice kilichopelekewa maji kwa mradi wa Bilioni 1.2

Rais Dkt John Pombe Magufuli wa pili kulia akizindua mradi wa Maji Kibamba Kisarawe uliojengwa kwa gaharama zaidi ya shilingi Bilioni 10.6,katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wameshiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...