Mchimbaji mdogo wa madini, Saniniu Kurian Laizer, akimkabidhi waziri wa madini Dotto Biteko mawe ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya  Shilingi Bilioni 7.74 katika hafla fupi iliyofanyika Mirerani.Pichani kati ni Naibu Waziri wa Madini  Mhe.
Stansalus Nyongo
Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof Simon Msanjila akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madini kutoka kwa mchimbaji mdogo wa Mirerani.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira (wa Pili Kushoto), Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula (Wa tatu kushoto) wakiwa na mchimbaji mdogo aliyegeuka kuwa bilionea Kurian Laizer (Wa pili Kulia) na Mchimbaji mdogo na Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi Thomas Munisi, eneo la Mirerani
Mkurugenzi wa Sheria katika wizara ya fedha, Elias Kimati (Kushoto), Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Adolf Ndunguru (wa pili kushoto) wakimsaidia Mchimbaji mdogo Kuriani Laizer (aliyevaa shuka la kimasai) kusaini fomu za mauzo ya madini yake ya Tanzanite
Naibu katibu mkuu, Wizara ya Fedha, Adolf Ndunguru, akimkabidhi madini yenye thamani ya Bilioni 7.7 Gavana wa Benki Kuu, Prof Florens Luoga
Waziri wa Madini Dotto Biteko akisikiliza simu aliyopigiwa na Rais John Magufuli kumpongeza mchimbaji Kurian Laizer katika mkutano wa hadhara.
PICHA ZOTE NA PAMELA MOLLEL
 
******************************


Na Pamela Mollel – Mirerani

Mkazi wa Mirerani, wilayani Simanjiro, Saniniu Kurian Laizer, ameibuka bilionea mpya mjini baada ya kufanikiwa kupata madini aina ya Tanzanite ambayo yamenunuliwa na serikali kwa gharama  zaidi ya shilling Bilioni 7.74.

Rais John Pombe Magufuli kupitia simu aliyompigia Waziri wa Madini, Dotto Biteko, amemsifu mchimbaji huyo mdogo, akisema kuwa amefurahi kuona watanzania wa kawaida sasa wameanza kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.

Biteko, pamoja na Naibu wake Stansalus Nyongo walikuwa wamehudhuria hafla maalum ya kumkabidhi mchimbaji huyo mdogo kitita hicho cha fedha, katika eneo la Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, siku ya Jumatano ya tarehe 24 Octoba 2020.

“Zamani tulitishwa kwa maneno ya uongo kwamba wachimbaji wadogo hawawezi kuzalisha kutokana na teknolojia duni, lakini Laizer hapa ameweza kuchimba kina cha mita 1800 na kupata madini haya, kwa hiyo Watanzania wanaweza,” alisema Biteko.

Naibu waziri Stanslaus Nyongo amesema kuwa yote haya yamewezekana kutokana na juhudi binafsi za Rais John Magufuli ambaye pia amefanikiwa kuzuia utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kwa kujenga ukuta mrefu wa Mirerani.

Nyong’o aliongeza kuwa sekta ya madini kwa sasa inakuwa kwa kasi kuliko sekta zingine nchini.

Naibu waziri wa fedha Ashatu Kijaji ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, ameongeza kuwa tangu miaka ya 80 wakati madini ya Tanzanite yalianza kuchimbwa, hayakuwahi kuwanufaisha wananchi wa kawaida hadi kipindi hiki.

“Hatujui huko nyuma tuliibiwa kiasi gani cha madini, lakini leo tunaona jinsi ambavyo watu kama Laizer wananufaika na hapa tunamkabidhi fedha zake zote kupitia mlipaji mkuu wa serikali,” alisema Kijaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...