LICHA ya baadhi ya safari na burudani kusimamishwa na shule tayari nchini zimefunguliwa, Shirika la ndege Emirates lenye urafiki na ukaribu na familia limezindua ukurasa maalum wa shughuli katika tovuti yake ili kuwaweka watoto kwenye burudani wakati wa likizo za majira ya joto.

Kupitia 'The Emirates Fly With me Animals' itawezesha  familia  ya kupata picha za kupendeza za rangi, hadithi na shughuli zilizo na sura za kirafiki na zinazojulikana na  kuleta faraja majumbani mwao.

 Miongo kadhaa ya kufanya kusafiri kwa ndege ya Emirates kumekuwa kwa  kufurahisha abiria na kuipa hadhi ya kuwa ndege kubwa ya kimataifa ya ulimwengu yenye utajiri wa uzoefu katika kutunza watoto wakiwa na furaha na salama.

Wazazi na watoto wanaweza kupakua na kuchapisha kurasa 16 za kitabu kupitia  'Fly with Me Animals" na kufurahia visa vingi vikiwemo  Lewis the Lion, Peek Uthe Panda, Ernie the Penguine, Savannah the Elephant, Elephant Brett the Bear Mia the Manta Ray na ChakChao the alligator.

Emirates imezishuri familia kuungana na  marafiki kwa kutuma ujumbe maalum kwa wale walio karibu na mbali, kwa kutumia moja ya kadi za posta zinazoweza kupakuliwa kwa urahisi au kuweka picha za wanyama wanaowapenda vizuri katika frame.

Watoto pia wanaweza kujifunza kupika mapishi ya kuoka ikiwemo  kwenda kutalii kupitia  Wanyama wapatikanao katika safu ya video za watoto.

Jarida la shughuli za Wanyama pia linapatikana kupakua na kila toleo limesheheni chemshabongo  na michezo ya kujifunza kufurahisha na kwa wale  wanakosa kusafiri  bado wataweza kutembelea maduka rasmi ya Emirates kununua vitu vya kuchezea nyumbani.

Imeelezwa kuwa programu hiyo ni muhimu  kwa likizo za majira ya joto na ni nafasi nzuri kwa watoto kupata ubunifu wa ziada na kugundua njia za kkujifunza wakiwa  nyumbani na kufurahia.

 Mwaka  jana, Emirates ilitoa midoli ya watoto zaidi ya milioni 4 pamoja na  majarida na seti za penseli na rangi kwa ajili ya kuchora na kusisitiza kuwa  msimamo wao wa kusafiri na familia ulimwenguni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...