Yassir Simba, Michuzi Tv

Robo fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports imeshuhudia Young Africans ikitangulia katika hatua ya nusu fainali na kuwangoja Azam, Ndanda, Simba pamoja na Sahare All Stars ya mkoani Tanga.

Katika Mchezo uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Yanga iliwakaribisha Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera katika hatua ya robo fainali.

Mchezo huo uliokuwa wa kasi na mvuto wakati wete, uliwawezesha Kagera kupata bao katika dakika 20 ya mchezo kupitia kiungo wake Awesu Awesu baada ya kupokea pasi ya kisigino kutoka kwa mfungaji bora wa kikosi cha Kagera Sugar, Yusuf Muhilu, na mnamo dakika ya 52 Yanga wakasawazisha kupitia Papa Molinga Falcao.

Dakika 72 ya mchezo Yanga walipata penati mara baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kufanyiwa madhambi na beki wa Kagera Sugar, Juma Nyosso na muamuzi wa mchezo huo kutoka Kigoma Shomary Lawy kuamuru Yanga kupiga penati kupitia kwa mchezaji wake, Deus Kaseke na kuipata Yanga bao la ushindi katika mchezo ambao pia uliwashuhudia Kagera wakicheza pungufu mara baada ya kiungo na mfungaji wa bao kwa upande wa Kagera Awesu Awesu kupata kadi  nyekundu  katika dakika 78 ya mchezo baada ya kupata kadi ya njano ya pili.

Rasmi sasa Yanga na Namungo Fc wanatangulia nusu fainali wakiwasubiri washindi katika michezo kati ya Azam Fc Vs Simba pamoja na Sahare All Stars Vs Ndanda ya mkoani Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...