Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Chiristopher Ole Sendeka,amepokea msaada wa fedha shilingi milioni mbili zilizotolewa na ujumbe wa viongozi wa dini wa kanisa la Tanzania assemblies of God (TAG) jimbo la Njombe kusini, uliongozwa na askofu wa jimbo hilo, Phairod Nyagawa kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na virusi vya Corona.
“Kwa hiyo nalipongeza kanisa kwa kumuunga mkono Mh.Rais katika msimamo aliouchukuwa”alisema Ole Sendeka mara baaa ya kukabiiwa fedha
Vile vile Kufuatia agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutaka shule zote za msingi na sekondari zifunguliwe juni 29, mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Njombe, Christoipher Ole Sendeka ameagiza shule za msingi na sekondari zihakikishe zinaendelea kuwa na kamati ndogo za afya zitakazohakikisha zinachukua hatua stahiki ya kusimamia wanafunzi wanazingatia ushauri wa wataalam wa afya wa kujikinga na ugonjwa CORONA
“Tupokwenda kufungua shule nachukuwa nafasi hii kuwaagiza wakuu wa wilaya,na wakurugenzi pamoja na waganga katika halmashauri zetu,kuhakikisha kila shule na taasisi za elimu ziendelee kuwa na kamati ndogo za afya zitakazokuwa zinatoa elimu kwa faia ya vijana wetu”alisema Sendeka
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Njombe, amelishukuru kanisa la TAG mkoa wa Njombe kwa dhamira yao ya dhati waliyoionyesha ya kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na janga hilo
Naye  askofu wa kanisa la TAG jimbo la Njombe kusini Phairod Nyagawa ameipongeza na kuiunga mkono serikali kuhusu mikakati iliyowekwa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa corona,bila kuathiri shughuli za kiuchumi za wananchi.
“Jimbo la Njombe kusini tunaungana na serikali kwa kutoa shilingi milioni mbili ili uongozi wa  mkoa uangalie namna unavyoweza kuhakikisha unasaidia katika mapambano dhii ya Covid-19”alisema  Phairod Nyagawa askofu wa kanisa la TAG jimbo la njombe kusini
Kutolewa kwa msaada huo ni hatua mojawapo ya mwitikio chanya wa mashirika na taasisi za kidini mkoani Njombe kujitokeza kutoa msaada wa hali na mali,lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na CORONA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...