Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
WATUMISHI saba wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) pamoja na Wakili wa Kujitegemea kutoka Kampuni ya Mnengele &Associates na ELA Advocatee watafikishwa mahakamani wakati wowote kwa kushtakiwa kwa tuhuma za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Hayo yameelezwa leo Juni 12 mwaka 2020 na Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza Daud Ndyamukama kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo amefafanua watumishi hao tayari wameshafukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria na wakati wowote watafikisha mahakamani kujitubu tuhuma zinazowakabili.
Ametaja tuhuma zinazowakabili ni tuhuma za rushwa , uhujumu uchumi pamoja na wizi wa wa fedha zaidi ya Sh.bilioni nane mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA. Watuhumiwa hao waliokuwa wanachunguzwa na TAKUKURU makao makuu ni aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao Makuu Deogratius Lema na aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao MakuuAike Mapuli aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao.
Wengine ni aliyekuwa Ofisa Uhasibu TPA Makao Makuu Marystella Minja, aliyekuwa Mhasibu wa Kituo cha Bandari ya Mwanza Thomas Akile, aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa Kituo cha Bandari Mwanza Ibrahim Lusato na aliyekuwa Keshia wa kituo cha bandari Mwanza Wendelin Tibuhwa, aliyekuwa Ofisa Kodi wa Kituo cha Bandari Mwanza James Mbedule pamoja na Wakili wa kujitegemea kutoka Kampuni ya Mnengele &Associates na ELA Advocatee Leocard Kipengele .
Kwa mujibu wa Ndyamukama ni kwamba watuhumiwa hao watasomewa mashtaka yao katika Mahamaka ya Hakimu Mkazi Mwanza wakati wowote."Nichukue fursa hii kutoa mwito hasa kwa watumishi wa umma mkoani Mwanza kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika utendaji wao wa kazi wa kila siku na kujiepusha na tamaa za mali na utajiri wa haraka".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...