TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashataka imemfungulia mashtaka Afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Peter Paul Sanga na msaidizi wa hesabu wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani Gothard Garfred Mbawala katika kesi ya uhujumu uchumi.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu washtakiwa hao walisomewa mashtaka hayo na wakili wa TAKUKURU Adam Kilongozi, mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Charles Uiso.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu washtakiwa hao walisomewa mashtaka hayo na wakili wa TAKUKURU Adam Kilongozi, mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Charles Uiso.
Makungu alisema washtakiwa hao walifanya ubadhirifu kinyume na kifungu namba 28 (1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Alisema katika kesi hiyo namba 07/2020 washtakiwa hao waliisababishia serikali hasara ya kiasi cha shilingi 1,040,000 kinyume na aya ya 10 (1) ya jedwali la 1 na vifungu namba 57 (1) na 60 (2).
Alisema washtakiwa hao walifanya udanganyifu katika utoaji wa leseni za biashara walizozitoa kwa wafanyabiashara mbalimbali wa mji wa Mirerani kinyume na kifungu namba 22.
Alisema washtakiwa hao waligushi leseni za biashara kinyume na vifungu vya 333, 335 (a) na 337 vya kanuni ya adhabu sura ya 20 ya mwaka 2002.
Hata hivyo, washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na waliweza kutimiza masharti ya dhamana na kuwa nje. Hakimu wa mahakama hiyo Uiso, aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 02 mwaka huu itakapokuja kwa hatua ya usikilizwaji wa awali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...