Na Stella Kalinga,
Simiyu RS.
Kituo cha utafiti wa kilimo nchini (TARI) kimechagua eneo la
viwanja vya maonesho ya nane nane vilivyopo kata ya Nyakabindi
wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa kituo endelevu cha uenezaji wa teknolojia
lengo likiwa kuwawezesha wakulima kupata huduma za kilimo kwa mwaka
mzima.
Hayo yamebainishwa na Bibi. Mshaghuley Ishika kutoka TARI Dodoma
kwenye kikao cha maandalizi nane nane kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye
jengo la mkoa wa Simiyu lililopo kwenye viwanja hivyo kikwahusiaha viongozi wa
Kanda ya ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga).
Aidha, Ishika amesema kituo hicho kitawarahisishia wakulima
kupata bidhaa zinazozalishwa kwenye Kituo hicho ambapo kwa hapa nchini
huzalishwa katika vituo 17, huku
akibainisha kuwa TARI kwa kutambua hilo wameamua kuongeza eneo la vipando katika
Viwanja vya Nyakabindi na kufikia hekari 3.
"Mbali na kuwa kituo endelevu cha usambazaji teknolojia kutakuwa
vifaa na duka la mbegu zinazozalishwa na TARI ambazo zinapatikana katika
vituo 17 hapa nchini na litamsaidia mkulima kujifunza mengi kuhusiana na
kilimo; kituo hiki pia kimepatiwa mtumishi wa kudumu atakayekuwa anasambaza
teknolojia kanda ya ziwa Mashariki ," amesema Ishika.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amesema maandalizi ya Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yamefikia
70% na kuongeza kuwa kwa upande wa vipando vimefikia 75%.
Wakati huo huo Sagini
amewaomba viongozi wote wanaotoka kwenye mikoa inayounda kanda ya
ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga) wakiwemo wakuu wa wilaya na
wakurugenzi watendaji kuhudhuria kikamilifu kwenye vikao vya maandalizi
ili yale wanayokubaliana wayatekeleze kwa wakati.
Akizungumzia masuala ambayo bado yanafanyiwa kazi Sagini amesema
kwa sasa kamati ya maandalizi inaendelea na ni ukarabati wa miundombinu
ikiwemo maji ,barabara na umeme huku akiwaomba washiriki kutoa
michango yao mapema ili kufanikisha maandalizi kwa wakati.
Awali akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mara,Mhe.Adam Malima,
Mkuu wa wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri ambaye pia alikuwa
Mwenyekiti wa kikao hicho, ameuhakikishia umma kuwa Maonesho ya Nanenane mwaka
2020 yatakuwa bora zaidi na yataacha alama; kutokana na maonesho hayo kufanyika kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo
katika kanda ya ziwa Mashariki.
Katika hatua nyingine mhandisi Msafiri amezitaka
halmashauri zote ambazo hazijaanza na zile ambazo maandalizi yake
yanaenda taratibu, kuharakisha kusimamia maandalizi hayo na kuhakikisha
yanakuwa ya kuridhisha, ili wakulima watakapokwenda kujifunza waone umuhimu wa
kilimo chenye tija.
Kanda ya ziwa Mashariki inaundwa na mikoa mitatu ambayo ni Mara,
Shinyanga na Simiyu na mwenyeji wa
maonesho ya Nane nane kitaifa ni mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo sasa,
ambapo kwa mwaka 2020 kaulimbiu ya
maonesho haya ni "KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Mhandisi. Mtemi Msafiri aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam
Malima akifungua kikao cha maandalizi ya Maonesho ya Nanenane kitaifa
mwaka 2020 ambayo yanafanyika kwa mara ya tatu mfululizo sasa katika
kanda ya ziwa Mashariki viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha
maandalizi ya maonesho ya nanenane kitaifa mwaka 2020 ambayo yanafanyika
kwa mara ya tatu mfululizo sasa katika kanda ya ziwa Mashariki viwanja
vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu wakifuatilia kikao hicho
kilichofanyika katika Viwanja hivyo Juni 15, 2020.

Bibi. Mshaghuley Ishika kutoka
TARI Dodoma akitoa taarifa katika kikao cha maandalizi nane nane Kitaifa
mwaka 2020 kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye jengo la mkoa wa Simiyu
lililopo kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha
maandalizi ya maonesho ya nanenane kitaifa mwaka 2020 ambayo yanafanyika
kwa mara ya tatu mfululizo sasa katika kanda ya ziwa Mashariki viwanja
vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu wakifuatilia kikao hicho
kilichofanyika katika Viwanja hivyo Juni 15, 2020.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akizungumza jambo na baadhi ya watendaji wa kanda ya
ziwa mashariki mara baada ya kikao cha maandalizi ya maonesho ya
nanenane Kitaifa mwaka 2020 ambayo yanafanyika kwa mara ya
tatu mfululizo katika kanda hiyo viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani
Simiyu wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika Viwanja hivyo Juni
15, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.
Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha maandalizi nane nane
Kitaifa mwaka 2020 kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye jengo la mkoa wa
Simiyu lililopo kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na
Uzalishaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichangia
hoja katika kikao cha maandalizi nane nane Kitaifa mwaka 2020
kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye jengo la mkoa wa Simiyu lililopo
kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Meneja wa NMB Kanda ya
Magharibi, Bw. Sospeter Magese akichangia hoja katika kikao cha
maandalizi nane nane Kitaifa mwaka 2020 kilichofanyika Juni 15, 2020
kwenye jengo la mkoa wa Simiyu lililopo kwenye viwanja vya Nyakabindi
Bariadi Mkoani Simiyu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...