NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
KATIKA kuhakikisha Huduma ya umeme inafikia vijijini vyote nchini serikali imetenga Trilioni moja nchi nzima   kupitia wakala wa umeme vijijini(REA) nchini huku Mkoa wa Morogoro ukitengewa zaidi ya Shilingi Biioni 42.0  kwa ajili ya huduma hiyo ya umeme kwenye  Vijijini  85  katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza  na kwamba vijiji hivyo vimeshafikiwa na huduma hiyo na kwamba huduma hiyo itafikia  vimeshafikia vijiji   vyote mia moja sitini na tano  ifikapo mwezi juni.

Akizungumza wakati wa kukagua Miradi ya umeme Vijiji Kamishna Msaidizi wa umeme toka Wizara ya Nishati Mhandisi Inocent Luoga amesema kuwa huduma hiyo itafikia pia Wananchi katika vitongoji vilivyopo kwenye Vijiji hivyo.

Kwa upande wake Mhandisi Raymond Seya kutoka kampuni ya State Grid inayojenga umeme vijijini katika mkoa wa Morogoro amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Vidunda kuhakikisha wanakamilisha Mradi huo kwa wakati na kuomba ushirikiano toka kwa Wananchi huku Diwani wa Kata ya Vidunda Bw Godian Makoye akiahidi kushirikiana na kampuni hiyo kufanikisha mradi kwa kushirikisha wananchi kujitokeza nguvukazi ya kubeba nguzo hadi maeneo husika.

Nao Wananchi wa Kata hiyo akiwemo, Marietha Makseyo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Lazaro Kiboga wamepongeza hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kuleta maendeleo katika Kijiji hicho kwani huduma hiyo waliokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.

Ziara hiyo imeshirikisha watendaji kutoka shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(Tanesco) likiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo ,wakala wa umeme vijijini(REA)na maafisa kutoka wizara ya Nishati ambapo watetembelea miradi ya umeme vijijini katika wilaya za Kilosa,Ulanga,Kilombero,Mailinyi,Gairo,Mvomero .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...