Balozi wa India nchini
Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu siku ya kimataifa ya mchezo wa Yoga ulimwenguni ambayo
hufanyika kila Juni 21 ya kila mwaka ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha
Watazania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili.Wengine ni Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto) na Balozi Msaidizi wa
Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(kulia).
Balozi wa India nchini
Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akifafanua jambo kuhusu
Siku ya kimataifa ya Yoga ambayo hufanyika kila Juni 21 ya kila mwaka. Wengine
ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto),Balozi Msaidizi wa
Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(aliyevaa suti ua bluu) na kulia
ni Katibu Raj Ganger.
Balozi Msaidizi wa
Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(kushoto) akizungumza kuhusu
Siku ya kimataifa ya Yoga ambayo inaratajia kufanyika Juni 21 mwaka huu.Kulia
ni Katibu wa Pili katika ubalozi huo Raj Ganger.
Balozi wa India nchini
Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli akizungumzia umuhimu wa kufanya
mazoezi kwa ajili ya kuuweka mwili katika hali nzuri kiafya huku akiwa amekunja
mguu kama ishara ya kuwa vizuri katika eneo la mazoezi.
Mkurugenzi wa Kituo cha
Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth
Raja(kushoto)akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kushiriki mashindano ambayo
yamedaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kuelekea siku ya kimataifa ya
mchezo wa Yoga.Wengine ni Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India
nchini Sanjiv Kohli, Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa India nchini Tanzania
R.Chandramouli(kulia), na mwisho kulia ni Katibu wa Pili katika ubalozi huo Raj
Ganger.
Balozi wa India nchini
Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akielezea jambo kuhusu
siku ya Yoga leo Juni 17,2020 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India nchini
Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(wa pili kushoto waliosimama juu)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandhishi wa habari waliosimama
chini pamoja na maofisa wengine wa ubalozi huo nchini.
Mkurugenzi wa Kituo cha
Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth
Raja(kushoto) akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu
siku ya kimataifa ya Yoga ulimwenguni.Kulia ni Balozi wa India nchini Tanzania
Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIKA kuelekea Siku ya Kimataifa ya mchezo wa Yoga ulimwenguni
kote ambayo ni Juni 21 mwaka huu, Ubalozi wa India nchini Tanzania
umewahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazeozi kwani yanafaida
kubwa mwili ikiwemo ya kuongeza kinga ya mwili.
Mbali na kuhamasisha watu kufanya mazoezi , Ubalozi huo umeeleza
ili kufanikisha siku hiyo ya Yoga wameandaa shindano la mazeozi pamoja na
kuhamasisha Watanzania kushiriki kwa kutuma video fupi fupi zinazoonesha
wakifanya mazoezi na washindi watashinda fedha taslimu ambazo zitatolewa na
Balozi wa India nchini Tanzania Sanjiv Kohli,
Hata hivyo kwa safari hii katika kuadhimisha siku hiyo ule
utaratibu wa maelfu ya watanzania kukutana na viwanja vya Uhuru jijini Dar es
Salaam na kushiriki mchezo wa Yoga kwa pamoja hautakuwepo kutokana na janga la
Corona ambalo limesumbua duniani kote.Hivyo safari hii Yoga itafanywa na watu
katika maeneo yao yakiwemo ya nyumbani.
Akizungumza leo Juni 17,2020 ,Balozi wa India nchini Sanjiv
Kohli ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa mchezo wa Yoga ambao kila
ifikapo Juni 21 ya kila mwaka huadhimisha katika mataifa mbalimbali
duniani."Niendelee kutoa rai kwa wananchi wa Tanzania kuungana na wananchi
wa India kushiriki kwenye mchezo huu ambao umejizolea umaarufu mkubwa duniani
kote tangu ulipoanzishwa.
"Katika kipindi hiki ambacho Dunia inapita kwenye kipindi
cha janga la Corona, mazoezi ni muhimu sana na uanasaidia kuongeza kinga za
mwili na hivyo mwili kuna na uwezo wa kukabiliana na magonjwa na hasa
yanayoshambulia kinga za mwili,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami
Vivekananda Santhoth Raja amefafanua
zaidi kuwa washindi watakaopatikana
watapata fursa ya kushindanishwa kidunia.Shindano hilo litaendeshwa kupitia
mitandao ya kijamii ikiwamo ukurasa wao wa Facebook, Twitter na Instagram.
Raja ametaja kusara za mitandao yao ni https://www.facebook.com/IndiaIntanzania/,https:www.facebook.com/swami-Vivekananda-cultural-centre-Dar-es-Salaam-582559985117910.
Akielezea zaidi kuhusu shindano ya mchezo wa Yoga, Raja amesema
kwamba washiriki ni watu wa rika zote na jinsia zote, hivyo jukumu lao litakuwa
ni mshiriki kutuma video fupi ya dakika tatu ambazo zitakuwa zinaonesha
wanavyofanya mazoezi wakiwa nyumbani.
Ameongeza kuwa shindano
hili linatarajia kufanyika Jumapili ya Juni 21 mwaka huu na nchi mbalimbali
duniani zitashiriki."Hivyo tunaomba Watanzania kushiriki kwa wingi ,
zawadi mbalimbali na hasa za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi.Kutokana na
ukubwa wa siku ya kimataifa ya Yoga , mataifa 177 yamefadhili mashindano
hayo,"amesema.
Kuhusu zawadi za kwa washindi , Raja amesema kuwa washindi watapata
fedha kuanzia Sh.200,000 hadi 300,000 kulingana na rika na kutakuwa na mshindi
wa kwanza hadi wa tatu kila kundi kutokana na video fupi zitakazotumwa.
Wakati zawadi kwa washindi wa pili watapata fedha kuanzia Sh.
150,000 hadi 250,000 kulingana na kundi huku washindi wa tatu kwa kila kundi
watapa fedha Sh. 100,000 hadi Sh.200,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...