Watu watatu wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kughushi huduma mbalimbali za kiuhamiaji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo katika Ofisi ndogo za Uhamiaji Makao Makuu Dar se salaam, Msemaji mkuu wa Uhamiaji Mrakibu Paul John Mselle alisema, Watuhumiwa hao walikamatwa jana  Juni 16,2020 majira ya saa saba usiku katika eneo la Somanga Wilaya ya Kigamboni na Mbagala Wilaya Temeke katika Jiji la Dar es salaam .

Watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na oparesheni inayoendelea hivi sasa ya kuwasaka watuhumiwa wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuhamiaji.

Hii ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wageni kudai kuwa wanatapeliwa na baadhi ya watu wanaojitambulisha kama maofisa Uhamiaji na wanawapa huduma ambazo siyo stahiki. “Tulipowafanyia upekuzi watuhumiwa hao, tuliwakuta na vifaa mbalimbali vya kiuhamiaji” alisema 

Miongoni mwa vitu vilivyokamatwa ni pamoja na Mihuri 2 ya Uhamiaji inayotumika kugonga ndani ya pasipoti wakati mtu aningia na kutoka nchini (Exit & Entry stamp) ya nchi ya Afrika ya Kusini

Mihuri 2 ya Uhamiaji inayotumika kugonga ndani ya pasipoti wakati mtu aningia na kutoka nchini (Exit & Entry stamp) ya nchi ya Malawi, Mihuri 2 ya Uhamiaji inayotumika kugonga ndani ya pasipoti wakati mtu aningia na kutoka nchini (Exit & Entry stamp) ya nchi ya Mauritius, Mihuri mbalimbali 18 ya Idara ya Uhamiaji Tanzania, Pamoja na Vifaa vingine.

Mrakibu Mselle aliendelea na kusema kwamba, Kwa sasa watuhumiwa wote watatu (3) wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji na kwa kuwa makosa yao yanaangukia kwenye Uhujumu uchumi basi watakabidhiwa kwa vyombo vingine vya Dola kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha amewakumbusha watanzania na wageni kwamba huduma za kiuhamiaji zinapatikana katika ofisi za Uhamiaji zilizopo nchi nzima na si vinginevyo pia mtu anaweza kupata huduma hizo kupitia tovuti ya idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz.
Msemaji mkuu wa Uhamiaji Mrakibu Paul John Mselle

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...