Charles James, Michuzi TV

MAHAMAMA nchini zimetakiwa kupambana na vitendo vya rushwa ili kuzuia ucheleweshaji wa haki unaofanywa kwenye kesi na mashauri mbalimbali yanayofunguliwa.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Jaji Mkuu nchini, Prof Ibrahim Juma alipokuwa akifungua kongamano la wadau kujadili rushwa katika mfumo wa utoaji haki nchini.

Jaji Mkuu amesema amesema vitendo vya rushwa hushamiri zaidi katika taasisi zinazo chelewesha haki na hivyo kutaka hatua zaidi za mapambano dhidi ya rushwa kuchukuliwa.

Amesema moja ya sababu za rushwa ni taasisi zinazohusika na utoaji wa haki kuchelewesha maamuzi hivyo kufanya wananchi kuona kuwa wanatakiwa kutoa kitu ili maamuzi yafanyike.

“Mapambano dhidi ya rushwa yasifanyike kwasababu tu Takukuru ipo bali yawe ni sehemu ya maisaha yetu ya kila siku katika taasisi zetu ili kuweza kufanikiwa kuishinda rushwa.

Uzoefu unaonyesha kuwa rushwa haiwezi kumalizwa na mahakama pekee bali taasisi zote zinatakiwa kushirikiana ili kupunguza vitendo vya rushwa katika taasisi hizo au kuimaliza kabisa,” Amesema Jaji Mkuu.

Amesema wananchi wamekua na mitazamo na hisia tofauti juu ya rushwa katika taasisi mbalimbali nchini na hivyo juhudi kubwa zinapaswa kuchukuliwa ili kurudisha imani hiyo iliyojenga.

Jaji Mkuu nchini, Prof Ibrahim Juma 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...