Na Amkiri kilagalila,Njombe
MWENYEKITI wa umoja vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Theopister Mhagama ametoa rai kwa vijana wa chama hicho,kubadili mfumo wa siasa na kuacha siasa za fujo na matusi badala yake kufanya siasa zenye ustaarabu na wenye kuruhusu demokrasia.
Mhagama ametoa ushauri huo wakati akizungumzia mtazamo wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu hasa kwa vijana.
“Tunataka vijana kubadili mfumo wa siasa,tusifanye siasa za matusi na vijana wetu hatuwaruhusu kufanya hivyo,tuliona hata kwenye chaguzi za serikali za mitaa siasa zilizofanyika zilikuwa za kistaarabu mtu akishindwa anakubali ameshindwa na sio kufanya fujo”alisema Theopista Mhagama
Vile vile amewashauri vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM kujitokeza kwa wingi ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama chao
“Kwa hiyo rai yangu kwa vijana jinsi walivyohamasika katika uchaguzi wa serikali za mitaa,naomba wajitokeze vile vile kwenye uchaguzi huu wa mwaka 2020”aliongeza Theopista
Aidha Bi, Theopister ameongeza kuwa vijana wanatakiwa kuachana na nidhamu ya woga kwa kile kinachodaiwa vijana wanakurupuka badala yake amewataka wajiamini kwa kuwa wanao uwezo mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...