Wadau wa mazingira kutoka Shirika la FORUMCC wakiendelea na majadiliano leo Juni 25,2020 Mjini Morogoro ambao wamekutana kujadilia bajeti ya Wizara ya Nishati pamoja na jitihada zinazofanywa katika kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Sehemu ya wanachama wa FORUMCC wakiwa makini kufuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya nishati jadidifu pamoja na jitihada za Serikali katika kuendeleza sekta hiyo nchini ikiwa pamoja na fedha zinazotengwa kufanikisha kuendelezwa kwa nishati hiyo nchini.
Felister Kasuga(katikati)ambaye ni mdau wa mazingira kutoka Elink Consult LTD akifafanua jambo wakati wa majadiliano kuhusu nishati jadidifu pamoja na kuangalia bajeti ya Serikali ambayo inaelekezwa katika katika kuendeleza sekta ya nishati jadidifu.
Sehemu ya wadau wa mazingira wakiendelea na mkutano wa majadiliano leo Juni 25,2020 mjini Dodoma. Mkutano huo umeandaliwa na FORUMCC kupitia Mradi wake wa kuendeleza nishati jadidifu chini ya ufadhili wa Shirika la Hivos.

Mmoja wa wadau akichangia jambo wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wadau wa mazingira kujadili nishati jadidifu pamoja na kuichambua na kuijadili bajeti ya fedha ya Wizara ya Nishati ambayo inatangwa kwa ajili ya kuendeleza nishati ikiwemo ya sekta ya nishati jadidifu
Wadau wa mazingira wakiwa kwenye majadiliano kuhusu matumizi ya nishati mbadala pamoja na kuchambua bajeti ya fedha Wizara ya Nishati ambayo kwa sehemu kubwa wameipoingeza kutokana na kuendelea kuongezwa fedha kuendeleza nishati jadidifu nchini. 




Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

WADAU mbalimbali wa masuala yanayohusu mazingira na mabadiliko ya TabiaNchi wakiwemo wa Shirika la FORUMCC wamesema wanafurahishwa na juhudi za Serikali katika mipango na mikakati yake katika kuhakikisha matumizi ya nishati jadidifu nchini yanapewa kipaumbele.

Miongoni wa jitihada hizo za Serikali ni pamoja na kuongeza fedha katika Bajeti ya Fedha ya mwaka 2020/2021 kwa Wizara ya Nishati huku miradi mikubwa ya usambazaji wa umeme vijiji na ujenzi wa miradi mikubwa ya umeme ukiwemo wa Bwala la kufua umeme la Mwalim Nyerere katika mto Rufiji.

Hayo yamesemwa na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Mabadiliko ya TabiaNchi na Mazingira Abdallah Henku wakati akizungumza na wadau hao waliokuwa katika ziara ya kimafunzo inayohusu nishati jadidifu yaliyoandaliwa na FORUMCC kupitia ufadhili wa Shirika la Hivos ambalo limejikita katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia nishati jadidifu.

Henku amefafanua Serikali kupitia Wizara ya Nishati imekuwa na mikakati ya muda mfupi, kati na muda mrefu.Hivyo katika mwaka 2014/15 Wizara ya Nishati iliweka mkakati wa kuwa na asilimia 36 ya uwekezaji wa nishati jadidifu huku kwa mwaka 2020/2021 ifikia asilimi 50 ya nishati hiyo."Katika mpango huo mwaka 2025/2026 imejipanga kufikia asilimia 75 ya nishati yetu kutokana na nishati jadidifu,"amesema.

Pia amesema katika bajeti ya mwaka huu Serikali imewafurahisha wadau wa mazingira hususani katika fedha yote iliyopangwa zaidi ya Sh.trilioni 1.2 zilizowekwa katika wizara ya nishati asilimia 88 ya fedha hizo zimetokana na vyanzo vya ndani ya nchi.

"Yanayoendelea sasa hivi tunafurahi sana sisi wadau wa mazingira kupitia bajeti hii ya juzi inaonyesha ni namna gani nchi ilivyojipanga vizuri katika uwekezaji wa nishati mbadala. Aidha asilimia 12 ya mashirika mbalimbali ya kimataifa yameweza kuchangia fedha hizo.Tunaona nuru inakuja katika uwepo wa nishati jadidifu, "amesema.

Kwa upande wadau wa wengine wa mazingira wametoa pongezi kwa FORUMCC kwa namna ambavyo limekuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwa pamoja na kuandaa mafunzo mbalimbali na kutoa elimu kwa jamii kuhusu mbinu bora za kukabiliana na athari zinazojitokeza kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kufanyika kutoka na shughuli za kijamii.

"Tunatoa pongezi kwa FORUMCC kwa jinsi ambavyo imejipapambanua katika eneo hilo la mazingira, wamekuwa rafiki wa utunzazaji mazingira kwa vitendo.Wengi wetu tumekuwa watunzaji wa mazingira kutokana na mafunzo yao mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyaandaa kwa nyakati tofauti kwa ajili yetu.Tunaahidi kuendelea kushirikiana nao ili kufika lengo la kuiwezesha nchi ya Tanzania na Dunia kwa ujumla kuwa salama kutokana na kuendelea kutunza mazingira yanayotuzunguka na kuendelea kuhamasisha kupanda miti na kutoharibu mazingira hovyo,"amesema mmoja wa wadau hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...