Na Woinde Shizza, Michuzi Tv- Arusha

WAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wamefurahia uhamisho wa kikazi wa aliyekuwa Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna ambaye amehamishiwa katika chuo cha mafunzo ya Polisi CCP kuwa Ofisa Mnadhimu rasilimali watu,Fedha na vifaa mkoani Kilimanjaro.

Shanna ambaye alifanikiwa kutekeleza amri ya Rais John Magufuli ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa mkoani Arusha,wafuasi wa chadema wameonekana kuchekelea uhamisho huo wakidai kwamba kamanda Shanna aliwanyima Uhuru wa kujenga chama chao.

Hayo yameibuka baada ya kusambaa taarifa za Kamanda Shana kuhamishwa kikazi mitaa mingi ya jiji la Arusha walionekana wakipongezana wakidai jimbo la Arusha litarejea chadema kwa kishindo baada ya kamanda Shanna kuondoka.

"Huyu RPC alitunyima usingizi kabisa tumeshindwa kufanya mikutano hata ya ndani hata viongozi wetu wa juu wakija Arusha inakuwa ngumu kukutana ila kwa sasa baada ya kuhamishwa tunaraha sana na ubunge Arusha tutashinda asubuhi" alisema mwenyekiti wa chadema Kata ya Ngarenaro Mathayo Munisi

Kamanda Shanna ambaye amedumu mkoani Arusha kwa takribani miezi 16 tangu kuanza kazi Machi ,1mwaka 2019 akitokea makao makuu ya Jeshi la Polisi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kumaliza matukio ya ujambazi wa silaha ,mauaji ya kinamama katika kata ya Olasiti na uvunjaji wa Nyumba , unyang'anyi wa kutumia nguvu ,ujangili na biashara ya dawa za kulevya.

Kamanda Shana ambaye alikuwa mchamungu akifahamika zaidi kwa jina la Askofu ,amefanikiwa kujenga nidhamu ndani ya jeshi la polisi na kusimamia ujenzi wa nyumba za polisi baada kuungua moto,kufufua magari ya polisi yaliyokuwa yamekufa kupitia wadau wa jeshi hilo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi na viongozi
Waliokuwa wakifanyakazi na Kamanda Shana wamesikitishwa sana na hatua ya uhamisho wake wakidai kuwa wameondolewa jembe ambaye aliwapa ushirikiano wa kutosha pale waliokuwa wamepatwa na changamoto za kiusalama.

Shanna amejijengea umaarufu mkubwa mkoani Arusha kutokana na aina yake ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na jinsi alivyokuwa akipambana na matukio ya uhakifu na kupelekea kupendwa zaidi na watu wa aina mbalimbali.

Akizungumzia uhamisho huu aliekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alisema kuwa huu ni uhamisho wa kawaida tu ndani ya jeshi na la polisi haihusiani na masuala yoyote na alimshukuru sana IGP Sirro kwa kuamini kuwa bado anastahili kufanyakazi yoyote ya jeshi la polisi.

Kwa upande wake mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tausi Swalehe alimpongeza Rais magufuli kwa kazi alioifanya na kubainisha kuwa amefanya jambo jema la kusafisha mji haswa katika kipindi hichi tunachoelwkea katika uchaguzi mkuu.

Amesema Rais Magufuli alivyowachagua viongozi hawa aliona wanafaa kwa kipindi hichi kukaa katika mkoa wa Arusha na kufanya kazi na alivyowatengua ameona muda wao wa kuwatumikia wananchi wa Arusha umefikia mwisho ,huku akimtaka aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuendelea kufanya kazi Kam vile alivyokuwa anafanyanmkoani hapa.

"Shana alipoingia mkoani hapa kulikuwa na uhalifu mwingi sana, akima mama walikuwa wanabakwa ,vibaka walikuwa wengi sana kulikuwa na wale vijana wanaitwa tatu mzuka lakini ameweza kusafisha mji na sasa tunakaa kwa amani, hivyo nimpongeze naomba aendapo aendelee kufanya kazi hivyo hivyo,"alibainisha Glory Swai

Kwa upande wake Jane Edward mwananchi wa Kata ya Kati amesema amesikitika kuondoka kw kamanda Shana kwani aliweza kutokomeza uhalifu na aliwafanya wabalifu wagope kutokana na kauli mbiu zake alizokuwa alitumia kuwatishia wabalifu pamoja na majina mbalimbali alipokuwa akiyatumia kipindi alipokuwa akifanya misako yake ya waalifu Kama vile kujiita Chita pamoja na mengineyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...