Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAKADA 12 wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wameshajitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika 25,2020.

Hadi leo mchana huu wa Juni 19 mwaka 2020, aliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi, Balozi Alli Karume, Mbwana Yahya Mwinyi anayetoka Umoja wa Vijana wa CCM, Omar Sheha Mussa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha katika kipindi cha utawala wa Dk.Salmin Amour.

Wengine ni Waziri wa Maji katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa, Hajj Rashid Pandu ambaye yeye amejitambulisha kuwa ni Mkulima, Mbwana Bakari Juma, Waziri Kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha, Mwantum Mussa Sultan,Balozi Meja Jenerali mstaafu Issa Suleiman Nassoro,Mohhamed Jafar Jumanne pamoja na Mohammed Hijja Mohammed. 

Makada hao wa CCM waliochukua fomu hiyo kwa nyakati tofauti wameeleza sababu zilizowasukuma ambazo kuchukua kuwania nafasi hiyo.

Kila aliyechukua fomu hiyo anaonesha kuwa na matumaini makubwa kurithi kiti cha urais ambacho Rais Dk.Alli Mohamed Shein anakwenda kustaafu baada ya kumaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba ya kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 10.

Kwa Waziri Dk.Mwinyi yeye baada ya kuchukua fomu hiyo ya kuwania urais hakueleza chochote kwa madai ya kwamba atakuwa na cha kuzungumza baada ya kuipitia fomu hiyo kisha kujua yaliyomo na hatimaye kuijaza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...