Moja ya watalaam wa masuala ya kilimo biashara akielezea namna bora ya upandaji mgomba wakati wanachama wa FORUMCC walipokuwa kwenye ziara ya kimafunzo kutembelea katika moja ya shamba lililoko Chuo Kikuu cha Kilimo(SUA).
Baadhi ya wanachama wa FORUMCC ambao wako kwenye kwenye ziara ya kimafunzo mkoani Morogoro kujifunza namna ambavyo nishati jadidifu inavyoweza kutumika katika shughuli za kilimo kama njia mojawapo ya kukabilina na athari za mabadiliko ya tabianchi.Ziara hiyo ya kimafunzo imefanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo(SUA).
Mkurugenzi wa Shirika la FORUMCC Rebeca Muna(wa kwanza kulia) akiwa na wanachama wengine wa shirika hilo kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiwa kwenye mafunzo yanayohusu utumiaji nishati jadidifu katika shughuli za kijamii ili kupunguza uharibifu wa mazingira.
Mkurugenzi wa Ushirika wa Wajasiriamali wa Wanafunzi waliosoma Chuo kikuu cha Kilimo(SUGEC)mkoani Morogoro Revocatusi Kimario(aliyesimama)akizungumza na wanachama wa FORUMCC kuhusu umuhimu wa kutumia nishati mbadala katika shughuli za kilimo.
Rebeca Muna ambaye ni Mkurugenzi wa FORUMCC akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashauri wanachama hao kuwa mabalozi kwa wengine kuhusu nishati jadidifu na umuhimu wake katika kukabiliana na athari za madiliko ya tabianchi.
Mtalaam kutoka Ushirika wa Wajasiriamali wa Wanafunzi waliosoma Chuo kikuu cha Kilimo(SUGEC)mkoani Morogoro Joseph Masimba akielezea namna ambavyo wanatumia nishati ya umeme jua kwa ajili ya shughuli za kilimo biashara ambacho wanajihusisha nacho bila kuharibu mazingira.
Wanachama wa FORUMCC wakipata maelezo kutoka kwa mtalaam Joseph Masimba kuhusu namna nishati ya umeme unaotokana na jua unavyotumika kukausha viazi lishe ambavyo vinalimwa na SUGEC.
Joseph Masimba ambaye ni mtaalam wa kilimo biashara kutoka SEGEC akielezea bandal ambalo ni maalum kwa ajili ya kukausha mazao yanayotokana shamabani kwa kutumia nishati ya umeme jua ambayo ni rafiki wa mazingira.
Baadhi ya wanachama wa FORUMCC wakiangalia tanki la kuhifadhi maji ambayo yanavutwa kwa pampu zinazotumia umeme wa nishati ya umeme jua baada ya kumtembelea nyumbani kwa moja ya wakulima ambao wananuifaka na nishati mbadala katika shughuli za kilimo.
Sehemu ya wanachama wa FORUMCC wakiangalia jinsi pampu inayotumia nishati ya umeme jua kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji baada ya kutembelea kampuni ya Simu Solar inayojihusisha na utengenezaji wa pampu za maji zinazotumia nishati mbadala.
Rebeca Muna ambaye ni Mkurugenzi wa FORUMCC akiwa ameshika kiazi lishe kabla ya kwenda kukaushwa kwa kutumia nishati mbadala.

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Morogoro
WANACHAMA wa Shirika la FORUMCC kutoka mikoa mbalimbali nchini wamefanya ziara ya kimafunzo mkoani Morogoro kwa jili ya kujifunza namna nishati jadidifu inavyoweza kutumika katika shughuli za kilimo.
Mafunzo hayo ni muendelezo wa mkakati wa FORUMCC katika kuhakikisha wanachama wao na wadau wa mazingira kwa ujumla wanakuwa na uelewa mpana wa mbinu mbalimbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya TabiaNchi na hasa kuihamasisha jamii kutumia nishati jadidifu katika shughuli za kimaendeleo.
Wakiwa katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na FORUMCC kupitia Mradi wake wa Nishati jadidifu unaofadhilia Shirika la Hivos, wanachama hao wamekutana na watalaam wa kilimo biashara kutoka Ushirika wa Wajasirimali wa Wanafunzi waliosoma Chuo kikuu cha Kilimo(SUGEC) mkoani Morogoro.
Akizungumza kuhusu wanavyotumia nishati mbadala katika shughuli za kilimo, Mkurugenzi SUGEC Revocatus Kimario kuna kila sababu ya Watanzania kuona umuhimu wa kutumia nishati jadidifu katika shughuli za kilimo ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesisitiza katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wao wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ikiwemo utumiaji wa nishati ya jua,umwagiliaji kwa njia ya Matone pamoja na kutumia ardhi ndogo katika kilimo kwa kupata mazao mengi.
“Matumizi ya nishati jadidifu katika shughuli za kilimo zimekuwa zikisaidia kwa sehemu kubwa kutunza mazingira na hivyo tunashauri wakulima hasa vijana kujikita katika aina hiyo ya kilimo ili kuwa na mazingira rafiki kwa kizazi cha sasa na kijacho,”amefafanua.
Akifafanua zaidi kuhusu kilimo biashara Kimario amesema SUGEC wanajihusisha na kilimo katika mtazamo wa kibiashara zaidi ukingalinisha na wakulima wengine ambao bado wanalima kilimo cha mazoea kisicho na faida.
Hata hivyo amesema pamoja na kutoa elimu ya kilimo biashara kwa vitendo, wamekuwa na jukumu la kubadilisha mtazamo wa jamii hususani vijana kuhusu kilimo ambacho kimepita kwenye hatua tofauti tofauti za unyanyapaa na hivyo kusababisha wengi kukichukukia.
"Wapo ambao wanachukulia kilimo kama adhabu na ndio maana katika baadhi ya familia au hata shuleni, mtu anapokosea anapewa adhabu ya kulima.Hivyo kazi yetu ni kuondoa dhana hiyo ya kilimo kuonekana ni adhabu.
"Tunataka jamii kutambua kilimo ni taaluma na ili kupata matokeo chanya lazima watu wafundishwe jinsi ya kujihusisha na kilimo.Kazi yetu sisi ni kuwaambia watanzania na hasa vijana kuwa kilimo kinalipa na kilimo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,"amesema.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea katika kuhakikisha kilimo biashara kinapewa nafasi ,wamekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo yanayohusu kilimo hicho sambamba na kupeleka vijana katika mataifa mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi na kupata mbinu mpya za kutumia teknolojia za kisasa kuendeleza kilimo biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa FORUMCC Rebecca Muna amesema matarajio yao ni kuona wanachama hao wanakuwa mabalozi kwenye maeneo yao kuhusu yale ambayo wamejifunza kutoka watalaam wa SUGEC kuhusu umuhimu wa kutumia nishati mbadala.
Amefafanua kinachofanyika kwenye mafunzo hayo ni uwekezaji wa fedha nyingi umetumika hivyo kila aliyepata fursa hiyo hakuna sababu ya kukaa kimya bali elimu hiyo kuipeleka ili ifike kwa wengine.
Ameongeza kuwa kitu cha msingi kila mmoja wetu analojukumu la kuhakikisha anakuwa sehemu ya kufanikisha matumizi ya nishati jadidifu katika kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...