Na Amiri kilagalila,Njombe
BARAZA la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Njombe Kwa Kauli Moja limeazimia kuwafuta kazi watumishi wawili kwa tuhuma za utoro kazini na kutoa barua ya onyo kwa wengine watano baada ya kamati ya maadili kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwakuta na tuhuma za uzembe zilizowafanya kukiuka taratibu za manunuzi.
Watumishi waliofutwa kazi ni Patrick Kigola mtendaji wa kijiji cha mfiliga pamoja na Asma Ally ambaye ni mtabibu ambao wanadaiwa kukutwa na makosa ya utoro kazini kwa zaidi ya miezi miwili na matumizi ya fedha za umma huku wengine 7 waliopewa barua ya onyo wakidaiwa kufanya uzembe na kukiuka taratibu wa manunuzi.
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza maalumu likiwa na agenda 15 ikiwemo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano cha 2019/2020 mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema timu ya uchunguzi kutoka kamati ya maadili imefanya uchunguzi usioacha shaka na kuamua kuwafuta kazi watendaji wawili na kutoa onyo kali la mwisho wengine saba.
“baada ya kamati ya maadili kujiridhisha na kamati ya uchunguzi kwa pamoja imeamua kuwafukuza kazi watumishi hao”alisema Valentino Hongoli
Akifafanua makosa yaliopelekea baraza kutoa uamuzi huo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ally Juma akasema ni utoro uliopindukia na kukiuka sheria na taratibu za manunuzi hatua ambayo imesababisha hasara serikali.
“Watumishi hawa wawili wamefukuzwa kazi kutokana na utoro kazini lakini kati ya watumishi watano,wanne ni maafisa ugani na mmoja ni mhandisi wamepewa onyo kutokana na uzembe na kukiuka taratibu za manunuzi”alisema Ally Juma
Kituo hiki kimezungumza kwa njia ya simu na Patrick Kigora afisa mtendaji aliyefutwa kazi na baraza la madiwani ambaye anasema kwa kuwa hana taarifa juu ya suala hilo hivyo hawezi kuzungumza chochote na anachojua bado ni mtumishi wa serikali.
“Kimsingi mimi hilo siwezi kulizungumzia mpaka nipewe barua rasmi,mimi natambua bado ni mtumishi wa serikali kwa hiyo siwezi kusema chochote kwa sasa”alisema Patrick Kigora
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...