WAZIRI  wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dk. Sophia Mlote kufuatia kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

 Mabadiliko hayo yamekuja siku chache baada ya Waziri Mpina kufanya ziara ya kushtukiza saa 10 usiku katika eneo Ubungo wanakouza maziwa
wajasiriamali wadogo na kupokea malalamiko ya wajasirimali hao
kuharibiwa maziwa yao kwa kuwekewa rangi na Mafuta ya taa na baadhi ya
maofisa wa Bodi ya Maziwa .

Hata hivyo Waziri Mpina aliagiza Maofisa wa Bodi ya Maziwa kusitisha mara moja operesheni ya kuharibu maziwa ya wananchi na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuwaelimisha namna bora ya kufanya biashara hiyo badala ya kuchukua uamuzi wa kuharibu maziwa yao kwa rangi na Mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo
Serikalini, Elibariki Mafole imesema uamuzi uliofanywa na Waziri Mpina
ni kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Maziwa namba 8
ya mwaka 2004.

Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Utafanyika hapo baadae.

Hata hivyo baada ya Waziri Mpina kufika eneo hilo la Ubungo alihoji hatua ya kuharibu maziwa ya wananchi kwa kuweka rangi na Mafuta ya taa
iliyofanywa na Bodi ya Maziwa ulizingatia Kanuni gani jambo ambalo
maofisa wa Bodi hiyo walioshindwa kuonesha kifungu kinachowapa mamlaka ya kupima maziwa kwa macho na kuweka mafuta ya taa.

Mmoja wa wafanyabiashara wa Maziwa, Ester Elius alisema zoezi hilo
lililofanywa la kuwawekea mafuta ya taa rangi kwenye maziwa limewapatia
hasara kubwa na kuomba Serikali kuwasaidia mikopo ili waweze kukidhi
matakwa ya kisheria yanayotakiwa na bodi hiyo badala ya  hivyo
Waziri Mpina aliagiza Mratibu wa Dawati la Sekta Binafsi la Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael kukutana na wajasirimali hao ili
kutambua mahitaji yao ya kifedha na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha
kwa ajili ya kupatiwa mikopo ili waweze kufanya biashara zao kwa tija.

Afisa wa Bodi ya Maziwa, Justa Kashumba alisema hatua walizochukua kuharibu maziwa hayo zipo kwa mujibu wa Kanuni huku akishindwa kumuonesha Kanuni iliyotumika Waziri Mpina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...