Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Maofisa wa Jeshi la
kujenga uchumi mara baada ya kuwatembelea kwa lengo la kukagua kambi
iliyokua ikitumika kwa kulaza wagonjwa wa Corona,hafla iliyofanyika
katika Ukumbi wa skuli ya JKU iliyopo Mtoni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed (kulia)akisisitiza jambo wakati
akiwa katika moja ya chumba kilichokua kikitumika kutoa huduma kwa
wagonjwa wa Corona Skuli ya JKU Mtoni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rshid Mohamed akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa
jeshi la kujenga uchumi Zanzibar [JKU] wakati akikagua maeneo
mbalimbali yaliyokua yakitumika kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohammed akikagua kituo cha
Afya cha Selemu Mfenesini ikiwa ni miongoni mwa vituo vilivyoteuliwaa
kutoa huduma za mwanzo kwa wagonjwa wenye dalili za Corona endapo
wakitokezea .
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohammed akiwa katika picha
ya pamoja na maafisa wa afya mara baada ya kukagua kituo cha afya cha
Fujoni ambacho ni
miongoni mwa vituo vilivyoteuliwa kutoa huduma za mwanzo kwa wagonjwa
wenye dalili za Corona endapo wakitokezea .PICHA NA-FAUZIA MUSSA/MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...