Waziri Zungu
akikagua bidhaa za Sufuria zinazozalishwa na kiwanda cha Ocean Alluminium
wakati alipofanya ziara kiwandani hapo. Picha na Charles Kombe
Waziri Zungu
akikagua baadhi ya nyaraka mbalimbali za kimazingira za kiwanda cha Ocean
Alluminium alipofika katika kiwanda hicho. Picha na Charles Kombe
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu (Kulia)
akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Ocean Alluminium,Dar es
Salaam. Picha na Charles Kombe
Mhe. Zungu
akiwasikiliza viongozi wa Kiwanda cha Ocean Alluminium akiwa Mkurugenzi Mkuu wa
NEMC Dkt. Samuel Gwamaka (Kulia) wakiwasikiliza viongozi wa Kiwanda cha Ocean
Alluminium wakati alipofanya ziara kiwandani hapo. Picha na Charles Kombe.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu
ametembelea kiwanda cha Ocean Alluminium kilichopo Tabata – Matumbi
kinachozalisha Sufuria ili kujionea uendeshwaji wa kiwanda hicho pamoja na
kutatua changamoto ya kukwama kwa mzigo wao.
Mhe. Zungu
akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka pamoja na wataalam mbalimbali wa Serikali,
amesema kuwa atakapofanya maamuzi ukaguzi wote stahiki utafanyika.
“Vyombo vya
ukaguzi tunavyo na pale tutakapofanya maamuzi hiki wanachokihitaji wamiliki wa
kiwanda hiki juu ya mzigo wao huu wa tani 40 hautatoka mpaka wataalam wetu
kutoka NEMC pamoja na wataalam wa mionzi kujiridhisha mzigo huu utakuwa ni
salama.” Amesema Mhe. Zungu
Akieleza kilichowapata hadi shehena yao kuzuiliwa
Bandarini Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Arman Arya amesema kuwa waliingiza
mzigo huo nchini bila ya kufahamu utaratibu unaopaswa kufuatwa.
“Tuliingiza
Kontena la malighafi bila ya kufuata taratibu za hapa nchini. Tulikuwa
hatufahamu juu ya taratibu hizo”. Amesema Arya, huku akiongeza kuwa baada ya
mzigo wao kuingia nchini ndipo walipofahamu juu ya taratibu hizo na wanamuomba
Waziri kama ikiwezekana awasaidie waupate mzigo wao uliokwama Bandarini.
Kutokana na
kupokea maombi ya Kiwanda hicho juu ya kupatiwa msaada kutokana na shehena yao
ya malighafi kukwama Bandarini, Mhe. Zungu amesema kuwa atashirikiana na vyombo
husika kulipatia ufumbuzi suala hilo.
“Tunachukua
malalamiko haya ambayo wameyaleta kwangu rasmi maana kwa mujibu wa sheria za
Nchi ni Waziri ndiyo mwenye mamlaka ya kushughulikia matatizo na kuhakikisha
kama kuna uvunjwaji wa sheria kitu gani kifanywe.” Amesema Mhe. Zungu, huku
akiongeza kuwa atashirikiana na Mkurugenzi wa NEMC, Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Makamu wa Rais na Wanasheria wa Serikali
kutizama namna tatizo hilo linaweza kutatuliwa.
Kwa upande
wake Aisha Omary, Meneja Uajiri katika kiwanda hicho anasema kuwa uzalishaji
umepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na kukwama kwa malighafi za kiwanda
hicho.
“Kiukweli
uzalishaji uko chini kutokana na kutokupatikana kwa malighafi lakini
tutakapopata malighali za kutosha tunatarajia tutazalisha kwa wingi.” Amesema
Aisha.
Kiwanda cha
Ocean Alluminium Ltd kinazalisha bidhaa za sufuria na soko lake kubwa ni katika
masoko ya Jiji la Dar es salaam huku kikiwa na wafanyakazi takriban 100 na
kinalipa kodi Serikalini kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...