Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiongea na Menejimenti ya Wizara kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kilimo IV Wizarani hapo.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akiwa pamoja na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri Mhe. Hussein Bashe na Kulia ni Naibu Waziri Mhe.Omary Mgumba wakiwa katika kikao cha menejimenti ya Wizara.
*******************************
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewaagiza watendaji Wakuu wa wizara na taasisi zake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu uzalishaji wa mazao na upatikanaji wa masoko ya uhakika.

Ametoa kauli hiyo leo (05 .06.20200 alipofanya kikao kazi cha menejimenti iliyohusisha wakurugenzi wa wizara,bodi za mazao na wakala zilizo chini ya wizara hiyo jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa kazi za wizara.

Hasunga amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano wizara ya Kilimo imefanikiwa kuimarisha uzalishaji wa mazao hususan ya chakula hali iliyopelekea nchi kuwa na utoshelevu wa chakula kipindi chote.

“ Wizara ya Kilimo imefanya mengi ya manufaa kwa kusimamia wakulima kuzalisha mazao mengi ya chakula na biashara hali iliyopelekea uchumi wa nchi kuimarika “ alisisitiza Waziri Hasunga.

Katika kikao hicho cha mwisho katika mwaka mwa fedha 2020 Waziri Hasunga alisema watendaji Wakuu wa wizara Taasisi watapimwa kwa kuongeza uzalishaji mazao ya kilimo ,pili idadi ya ajira zitakazozalishwa kwenye mnyororo wa thamani wa zao, Tatu mchango wa zao katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na nne idadi ya wakulima na kiasi cha ekari wanachozalisha.

Hasunga aliongeza kuwa Bodi za mazao zitapimwa kwa mashamba bora ya mfano waliyonayo,sita idadi ya viwanda vinavyochakata mazao ya Kilimo na mwisho idadi ya masoko kwa mazao ya wakulima.

Amezielekeza bodi za mazao na taasisi zote kuhakikisha zinaweka utaratibu mzuri wa kuepusha kero za wakulima kuhusu upatikanaji wa mbegu bora,pembejeo,viuatilifu na masoko ili wanufaike na kazi za Kilimo .

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza wizara ya Kilimo kuhakikisha inaondoa kero zote za wakulima kwa kuzitatua haraka katika ngazi zote hadi wilayani ili asiwepo mtu yeyote atakayekuwa kikwazo kwa wakulima nchini” amesisitiza Waziri Hasunga.

Katika kikao kazi hicho Waziri huyo wa amesisitiza kuwa serikali haitopanga bei za mazao ya pamba,mahindi mpunga au ufuta bali itahakikisha wakulima wanapata bei nzuri ya soko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema watumishi na watendaji wa wizara wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu ili wakulima nchini wanufaike .

Kusaya alisema ataendelea kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa watendaji wakuu na taasisi zake ili malengo ya Serikali na maagizo yote yapatiwe utekelezaji ili uzalishaji na tija kwa mazao ya wakulima nchini uongezeke.

Kikao kazi hicho kimehudhuriwa pia na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba ambao wametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi kwa ushirikiano walioutoa kwa Mawaziri kwa kipindi chote walichofanya kazi wizarani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...