Na Amiri Kilagalila, Njombe

Julai 14,2020 mshtakiwa Luka Nelikon Mahenge (18) mkazi wa kijiji cha Isapulano wilaya ya Makete mkoa wa Njombe amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete akituhumiwa kwa makosa mawili ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya Sekondari Iwawa (17).

Imeelezwa mnamo Julai 10,2020 majira ya saa 9 alasiri katika kijiji cha Iwawa kilichopo wilaya ya Makete Mkoani Njombe bila halali mshtakiwa alimbaka mwanafunzi Huyo jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Iwawa kinyume na kifungu namba 130 kifungu kidogo 1 na 2 [e] na kifungu cha 131 kifungu kidogo 1 vyote vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Pia mshtakiwa huyo amesomewa shitaka la Pili ambapo bila halali anashtakiwa kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) kinyume na kifungu namba 60 [A] kifungu kidogo cha 3 cha sheria ya elimu kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya bunge namba 2 ya mwaka 2016.

Aidha mshtakiwa huyo amekana makosa yote mawili na shauri hilo limeahirishwa na hakimu mfawidhi wa wilaya ya makete Mh John Mpitanjia chini ya mwendesha mashtaka Benstard Mwoshe kwa ajili ya usomaji wa hoja za awali mpaka Julai 21 2020. Hata hivyo mshtakiwa amepelekwa mahabusu baada ya Kushindwa Kukidhi masharti ya Dhamana ya kudhaminiwa kwa shilingi milioni 5.

Wakati huo huo mahakama ya wilaya ya makete imeendelea kusikiliza shauri namba 32 la jamuhuri dhidi ya Felix Zainab Sanga anayeshtakiwa kwa makosa mawili La Kubaka na Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Darsa la Saba katika shule ya msingi Igolwa (17) jina Linahifadhiwa ambapo shauri hilo limeahirishwa mpaka tarehe 20 Julai 2020 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...