Na Khadija Seif, Michuzi TV

MALKIA wa Muziki wa Bongofleva Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee amewataka mashabiki nchini wa muziki huo nchini kuacha tabia ya kuwapambanisha wasanii wenye majina makubwa dhidi ya wasanii wanaochipukia.

Jay Dee ambaye wakati mwingine huitwa Komando Jdee ,ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye siku ya Iam Zuchu ahsante nashukuru ambapo amesema wakati mwingine wasanii wanaochipukia wanakatishwa tamaa kutokana na tabia ya kupambanishwa na wakongwe.

Amefafanu sio sawa kumpambanisha msanii chipukizi dhidi ya msanii mkonge ambaye kwenye muziki  ameshafanya mambo makubwaa na wamepokelewa vizuri."Kuwapambanisha wakongwe na wasanii wanaochipukia sio sawa, wanaweza kuvimba kichwa na kulewa sifa."

"Minong'ono ilikuwa mingi mno kipindi naanza muziki, hivyo hata kwa zama hii nisingependa kuona hili tatizo linaendelea kwani tumepoteza wasanii wengi ambao wamekatishwa tamaa tu kutokana na mihemko ya wanahabari pamoja na mashabiki,tusiwafananishe tuwaache kila msanii ang'are kivyake ila  kazi zao zitaongea tu kwani kila mtu ana upekee wake,"amesema Jay Dee.

Kuhusu 'Show' ya Zuchu ambayo imeandaliwa na Lebo yake ya WCB kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki na Watanzania kwa ujumla kwa kumokea vizuri  Jay Dee amempongeza huku akimsifu kwa jinsi alivyo na nidhamu.

"Anaonekana ana nidhamu,uthubutu wa kuziishi ndoto zake, nimekutana nae tumeongea vingi na hakusita kuniambia kuwa alikua ana ndoto ya kukutana na mimi na ameishi kwenye ndoto hiyo hatimae imetimia.Namsihi  namsihi tu aendelee kukaza buti na atafika mbali anapopata hasa akilizingatia suala la nidhamu,"

Wakati huo huo Jay Dee amempongeza mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa kwa kumruhusu mtoto wake kuingia kwenye muziki.

"Ni wazazi wachache sana ambao wanaruhusu watoto wao kuingia kwenye shughuli za sanaa kwani sanaa mara nyingi kwa upande wa mabinti imekua na vikwazo vingi ambavyo ni wachache sana tulivishinda vikwazo hivyo na kufika hapa tulipo.Hivyo  kwa namna moja au nyingine mama Khadija anastahili pongezi na atakua ameshampa mawili matatu ambayo yatamjengea misingi mizuri kwenye sanaa ya Zuchu,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...