Charles James, Michuzi TV

ANASTAHILI Mitano tena! Ndio kauli ambayo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi ameitoa wakati akielezea kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk John Magufuli ndani ya uongozi wake

DC Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati alipokua kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana na Kamati ya Siasa na kukagua miradi mbalimbali ya Maji, Elimu, Afya na Kituo cha Polisi ambayo imegharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.7.

Amesema kwa miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake, Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania kwa kuwaletea maendeleo makubwa yaliyoenda sambamba na mageuzi ya kiuchumi na ndio maana Benki ya Dunia imeitaja katika orodha ya Nchi zenye uchumi wa kati.

DC Ndejembi amesema ndani ya Wilaya yake ya Kongwa, Serikali imepeleka miradi mikubwa ya kimaendeleo ambayo pia imekua msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

" Kongwa ya sasa hakuna changamoto yoyote katika sekta ya Afya, ujenzi wa Kituo hiki cha Afya hapa Mkoka ni kielelezo cha namna gani serikali yetu inajali Afya za wananchi wake, siyo hapa tu, ndani ya Wilaya yetu changamoto hii haipo tena.

Kwenye elimu serikali kwa kushirikiana na Mbunge wetu ambaye pia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja kuwa Kwa sasa kuna Sera ya elimu bila malipo bado madarasa mengi yamejengwa pamoja nyumba za walimu, yote hayo ni kuonesha jinsi gani tumeamua kuongeza kiwango cha ufaulu wilayani kwetu," Amesema DC Ndejembi.

Amesema zawadi pekee ambayo wananchi wa Kongwa wanapaswa kumpa Rais Magufuli kutokana na maendeleo hayo ni kumpigia kura nyingi za ndio yeye na Spika Job Ndugai ili waweze kuwatumikia tena kwa kasi katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wana CCM Wilaya ya Kongwa, amesema ni wazi macho yao yamejionea kazi kubwa iliyofanywa na Rais Magufuli kwenye wilaya yao ndani ya kipindi cha miaka mitano na kwamba atawaongoza vijana wenzake wa Kongwa kumpigia kura nyingi za ndio Rais na Mbunge Ndugai.

" Kuna msemo unasema kusoma hujui hata picha huoni? Sasa sisi vijana tunasema kwa maendeleo haya makubwa ambayo Rais Magufuli ameyaleta kwetu tutakua wenye dhambi sana kama Wilaya yetu haitoongoza kwa kura za ndio kwa Rais na Mbunge wetu," Amesema Mwenyekiti huyo.
 Mkuu wa Wilaya Kongwa,  Deo Ndejembi akiwa ameongozana na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo wakikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mkoka.
 Muonekano wa Kituo cha Afya Mkoka wilayani Kongwa ambacho kipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.
 Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kongwa ikiongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Deo Ndejembi wakikagua mojawapo ya nyumba za walimu ambazo zimejengwa kwenye Wilaya hiyo.
 Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kongwa ikiwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikikagua mradi mkubwa wa Maji ambao uko karibu kumalizika.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...