Afisa Mkuu wa biashara wa Emirates Adnan Kazim

BAADA Ya Shirika la ndege la kimataifa la Emirates huduma za safari Geneva kuanzia Julai 15, Los Angeles kuanzia Julai 22, Dar es Salaam kuanzia Agosti Mosi, Prague na Sao kuanzia Agosti 2 na Boston kuanzia Agosti 15 na kufanya shirika hilo kuifikia miji 58 hadi kufikia mwezi Agosti huku miji 24 ikiwa ya bara la Ulaya na miji 24 kutoka Asia.

Afisa mkuu wa biashara wa shirika Hilo Adnan Kazim amesema kuwa kumekuwa na mahitaji mengi ya safari kutoka kwa wateja wao tangu walipotangaza kurejesha safari za Dubai pamoja na kuunganisha maeneo mengine zaidi.

 Aidha amesema kuwa Emirates itaendelea kufanya kazi kwa karibu zaidi na wadau wao katika kurudisha huduma zote sambamba na kuimarisha huduma za afya kwa wateja na wafanyakazi wao.

Pia ameeleza kuwa  wateja wa Emirates wanaosafiri katika maeneo ya ukanda wa Ulaya, Afrika, Asia na Mashariki ya kati sasa wanaweza kufurahia safari zao kwa usalama zaidi na pia wateja wanaweza kupita au kutembelea Dubai kwa kuwa mji huo umefunguliwa kwa biashara za kimataifa na mapumziko kwa wageni.

Shirika hilo pia limewataka wateja kuendelea kuchagua kutoka Shirika hilo na kufurahia safari zao huku sera za kubadili safari zao zikielezwa kuzingatiwa.

Mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...