*Yaweza kupima sampuli nyingi kwa wakati mmoja na wataalam wapo wa kutosha
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)imesema kuwa kwa sasa ina wataalamu wa kutosha na mitambo ya kutosha ambayo inaweza kuchukua sambuli nyingi kwenda maabara.
Upimaji wa sampuli nyingi kwa wakati inarahisisha mamlaka kutoa huduma kwa wakati ikiwa ni kupunguza changamoto ya foleni kwa wananchi wanaohudumiwa na mamlaka hiyo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Sabanitho Mtega wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja wa maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mtega amesema Serikali imewapatia wataalamu wa kutosha ambayo kila kukicha wamekuwa wakipata ujuzi unaowawezesha kufanya kazi kwa weledi na kujitegemea katika kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha amesema majukumu ya mamlaka hiyo yametengwa katika maeneo matatu, ambapo eneo la kwanza ni huduma za kiuchunguzi wa sampuli mbalimbali, huduma za kisheria na utoaji wa ushahidi mahakamani pale linapokuwa limefunguliwa shauri.
Amesema katika eneo la huduma za kiuchunguzi wamekuwa wakifanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali kama vile dawa asili, vyakula, kemikali, viwatilifu pamoja na sampuli za mazingira na kuongeza kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo utoa majibu kwa ajili ya kusaidia mamlaka za udhibiti kufanya maamuzi stahiki.
Mtega amesema wamekuwa wakifanya uchunguzi wa sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, ambapo baada ya kuchunguza uwasilisha matokeo kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi ya kisheria.
"Pia sisi ni mamlaka ya udhibiti unaosimamia kemikali za majumbani na viwandani hivyo katika hali hiyo kemikali zote zinazoingia nchini lazima sisi kama mamlaka tuwasajili wale wote wanaoziingiza na kutoa kibali kwa ajili ya kusafirisha ndani na nje ya nchi kemikali hizo," amesema
Amesema kwa hali hiyo wamekuwa wakifanya ukaguzi kwa saa 24 kila siku na kuomgeza kuwa wana wakaguzi wao katika kila mipaka nchini kwa ajili ya kuharakisha utoaji wa mizigo na kuangalia kemikali zote zinazoingia nchini zina ubora unaokubalika na zinatumika kwa malengo yaliyoletewa na si vinginevyo.
" Bado tunayo changamoto kwenye uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli mbalimbali ambapo wengi wa wadau uleta sampuli kidogo lakini inahusisha vigezo vingi au kuletewa sampuli ambayo ilihifadhiwa bila kufuata utaratibu hivyo tunashundwa kulifanyia uchunguzi kutokana na kutokidhi viwango vya kufanyiwa
"Katika eneo hili tumekuwa tukiwasiliana na wadau na kuwaelimisha kwamba wanapaswa kuleta sampuli nyingine ili tuweze kufanya uchunguzi na kuwapatia majibu," amesema.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Sabanitho Mtega akizungumza kuhusiana na huduma mbalimbali wanazozozitoa pamoja na elimu katika maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanyofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Mkemia Mwandamizi wa GCLA John Wanjala akitoa maelezo kwa waandishi habari katika maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...