Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya Tatu, Willium Benjamin Mkapa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo, aliongea mambo mbalimbali katika nyakati tofauti.

Katika siku ya uzinduzi wa kigoda cha Mwalimu alisihi uwajibikaji wa wazazi katika elimu, katiba na sera za nchi.

"Nilipofika hapa nilifanya mkutano nje ya shule pia barabarani pale niliagalia nyumba zenu nyingine zina bati, nyingine zina nyasi lakini milango yote ni ya mbao, chanja za kuweka vyombo vya chakula nizambao, kuna viti nje watu wanakaa pale wanazungumza nikawaambia kama mnauwezo wa kufanya hayo kwanini mnashindwa kukusanya nguvu na kujenga uwezo wa kuwawekea watoto wenu madawati wasome vizuri". Alisema mkapa katika siku ya kigoda cha mwalimu Juni, 2016.

Hata hivyo Mkapa siku hiyo hiyo alizungumzia kuhusiana na sera za uchumi ambapo mpaka sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Joseph Pombe Magufulia anazungumza kila uchwao apatapo nafasi kuanzia uchumia wa viwanda na mpaka nchi yetu kutangazwa kufikia uchumi wa kati.

Hivyo Mareemu Mkapa alisema kuwa kampuni nyingi zimeanzishwa na watanzania kwani sheria zimetungwa na ruhusa ya kuanzishwa ipo.

Mkapa alihoji pia kuhusiana na mgogoro uliokuwepo kipindi yeye ni Mbunge wa kampuni moja ya simu wakati sheria na ruhusa ya kuanzishwa kampuni ipo.

"Mmeona kampuni kubwa ngapi zimeanzishwa na watanzania, mangapi? Na kinachozuia ni nini?sheria zimetungwa, ruhusa ipo lakini tunabaki kugombana na juu ya kampuni hiyo hiyo ya simu tunataka nayo iwe ya umma kusudi ishindane na hao wengine mtawaweza kweli?. Alihoji Mkapa.

Kuhusu sera
Alisema kuwa wananchi tunapenda kuzungumza watu badala ya sera na kuhoji ni wapi hasa sera hizi zinazungumzwa.

"Tunapenda kuzungumza watu badala ya sera! hatuwezi kuendelea namna hiyo wapi sera hasa zinazungumzwa hata sera ya elimu, au ya uchumi, ya afya wapi hasa inazungumzwa hatuwezi kuendelea kwa namna hiyo".
Alisema Marehemu Mkapa.

Tukitaka kuendana na sera ya Rais Magufuli havipishani sana na Marehemu Mzee Mkapa. Kwasasa tukiwa na Tanzania ya Viwanda.

Hata hivyo aliwasii viongozi wawe wasikivu kwani ndio sifa kubwa alikuwa nayo Mwalimu Nyerere. Mkapa pia alizungumzia kihusiana na uhuru wa kujieleza.

Marehemu Mkapa kwakuwa yeye alikuwa Mwandishi wa Habari Kitaaluma hakusita kuzungumzia uhuru wa kujieleza.

alisema kuwa magazeti ya serikali na ya IPP hayatoshi peke yake hivyo akamwomba Agha Khan kuanzisha magazeti mengine hapa nchini ya Mwananchi na The Citizen.

Hivyo kwa sasa tunaona utitiri wa magazeti kwa kuwa tuu Marehemu Mkapa aliona uhuru wa kujieleza uendane na maendeleo yaliyopo hapa nchini. 

Kuhusiana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa yeye hakuwa katika maamuzi yeyote wala hakuwa mshauri wa Rais na wala kwenye chama chake cha CCM hakuwepo na kwenye serikali hakuwemo kwahiyo hakuweza kutoa maoni yeyete siku hiyo ya Kigoda cha Mwalimu.

Licha ya hayo Marehemu Mkapa alihoji ni kwanini na kwa namna gani ile katiba ilikwama? 

Waandishi wa habari walitaka kujua mtazamo wake juu ya mchakato wa  Katiba Mpya uliokuwa  kuanzia 2013 hadi 2014 ambapo naye marehemu Mkapa hakuwa na maoni kwani hakuwemo katika nafasi yeyote.

Ambapo Mpaka sasa mchakato ule wa katiba mpya, kukusanya maoni pamoja na Bunge la katiba ndipo palipoishia.

Marehemu Mkapa enzi za uhai wake alionya kulaumiana na kudai ila kuwezesha Uhuru wa kujieleza pia kuutumia huo uhuru wa kujieleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...