Kamati yaMaudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Kwanza Online Tv kutochapisha habari kwa miezi 11 kuanzia Julai 6 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Joseph Mapunda amesema Kwanza Online TVJulai 1,2020 kupitia ukurasa wa Instagram walichapisha taarifa inayodaiwa kutolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
iliyojaa upotoshaji kwa jamii bila kutafuta usahihi na ukweli wa taarifa
husika,na bila ya kuzingatia mizania ya Habari.

Mapunda amesema  Kwanza Online TV ilichapisha maudhui hayo yaliyokuwa katika mfumo wa picha mnato,ambayo yanadaiwa yanatoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania .
 
Amesema katika utetezi wake wa  maelezo ya kimaandishi yaliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Maudhui,uongozi wa Kwanza Online TV uliiambia Kamati kuwa Kwanza Online TV inapinga mashtaka husika kwani Kwanza
OnlineTV imetoa taarifa inayotimiza matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania chini ya Ibara ya 18, inayompa mtu uhuru wa
kutoa maoni yoyote, kutoa mawazo yake kutafuta kupokea kutoa
habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi.

Kamati katika maelezo ya Uongozi wa Kwanza Online TV uliiambia
Kamati kuwa walichapisha habari hiyo kwa lengo la kuujulisha umma
juu ya maoni ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,kuhusu ugonjwa wa COVID-19 na kuendelea kudai kuwa kwa asili ya habari hiyo ni
kwamba haikuwa na mantiki wala haja ya kutafuta upande wa pili
kwani taarifa hiyo ilikuwa ni taarifa kwa umma na siyo aina ya taarifa
ambayo inahitaji upande wa pili kwa sababu yale yalikuwani maoni na
msimamo wa Ubalozi wa Marekani na hata kutafuta na kupata maoni upande wa pili kusingeweza kubadili maudhui ya taarifa ambayo
imechapishwa na Ubalozi wa Marekani.

Amesema uongozi wa Kwanza Online TV ulidai kuwa uzalendo
wa ulikuwa ni kuujulisha umma kuwa mataifa mengine yanazungumza
nini kuhusu nchi yaTanzania ,na ni hatua gani nchi yetu inatakiwa
ichukue ili kuepuka minong’ono kutoka mataifa mengine.
Pamoja na utetezi wao.

Amesema  baada ya kupitia kwa umakini na kutafakari kwa kina maelezo ya
utetezi wa maandishi uliotolewa na Uongozi wa KwanzaOnlineTV,
Kamati ya Maudhui imeridhika pasinashaka kuwa Kwanza Online TV
kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wa Instagram imekiuka
Kanuni Na.7(1)(a),(b)na12(l)za Kanuni za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta(Maudhui ya Mitandaoni),2018pamoja na
Kanuni Na.11(1)(a)na15(2)(b)na(c)za Kanuni za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta(Maudhui ya Utangazaji wa Redio naTelevisheni),
2018.
.
Hivyo basi,kwa mujibu wa Kifungu cha 28(1)(b)na(d)chavSheria ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Sura ya 172 ,Marejeo ya Mwaka
2017.


Makam Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joseph Mapunda akisoma hukumu ya Kwanza Online Tv na kuifungia miezi 11 ya kutotoa huduma .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...