Mkurugenzi wa uendeshaji UTT-AMIS Issa Wahichindena akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kuhudumia wawekezaji cha UTT-AMIS katika jengo la Ngorongoro, jijini Arusha, anayeangalia (Katikati) ni meneja wa uhusiano katika kitengo cha uangalizi wa amana katika benki ya CRDB, Mary Mponda (Picha na Pamella Mollel).
 Picha ya Pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa UTT-AMIS na wafanyakazi wa benki ya CRDB mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kuhudumiawawekezaji Arusha (Picha na Pamella Mollel)
 Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga akizungumza na waandishi wa habari wa kati wa hafla hiyo (Picha na Pamela Mollel)
 Meneja wa Uhusiano, kitengo cha uangalizi wa amana, katika Benki ya CRDB Mary Mponda (Kulia), akizungumza katika uzinduzi wa UTT Arusha, huku Meneja wa Tawi la TFA la benki ya CRDB Arusha Ronald Paul (Kushoto) akifuatilia kwa makini (Picha na Pamella Mollel)



Na Pamela Mollel, Arusha

Kampuni ya Serikali inayohusika na Uanzishaji na Uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini, UTT-AMIS imezindua tawi lake la tatu jijini Arusha baada ya lile la Dodoma katika mkakati wake wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

“Tunafungua rasmi kituo cha kuhudumia wawekezaji wetu katika jiji la Arusha, hii ni ikiwa ni ushahidi wa maendeleo mazuri katika sekta ya uwekezaji kwa wananchi wa kawaida, Tanzania zikiwa ni juhudi kubwa za serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Maguifuli,” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji wa UTT-AMIS, Issa Wahichindena.

Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho katika jengo la Ngorongoro Conservation Center, lililopo katikati ya jiji, Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa kuwekeza katika mifuko hiyo wawekezaji wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji.

Naye mkuu wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga amesema kuwa kuna umuhimu wa wananchi kuongeza thamani ya akiba zao kwa kuwekeza fedha katika mifuko ili kupata faida kubwa badala ya kuziacha benki ambako riba zake huwa ndogo.

Katika uzinduzi huo pia walikuwepo maafisa watendaji wa benki ya CRDB, akiwemo Meneja wa Uhusiano, kitengo cha uangalizi wa amana, Mary Mponda ambaye alisema kuwa taasisi yao kwa sasa ina matawi zaidi ya 280 nchini kote na kuwa katika nafasi nzuri ya kusimamia mifuko ya uwekezaji nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...