KAMPUNI ya wa Asili Asilia inawakaribisha wananchi wote ambao wanakuja kwenye maonyesho ya sabasaba katika Banda la karume ili kujipatia bidhaa mbalimbali za ngozi ikiwamo viatu vya kisasa,mabegi,mifuko,mikanda.

Akizungumza katika Viwanja hivyo vya maonesho  ya 44 ya sabasaba leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Denan Munis amesema anawakumbusha watanzania kwamba huu hi wakati wao wa kuonyesha uzalendo Kwa kutembelea mabanda ya bidhaa zinazotengenezwa na watanzania.

Amesema kuwa kitendo cha kuunga mkono kwa kununu bidhaa zinazotengenezwa na watanzania niwazi kwamba unachangia uchumi wa nchi lakini pia kuongeza kutoa ajira Kwa vijana wakitanzania.

"Nawakaribisha Sana kwenye Banda letu hili la maonyesho ya sabasaba jengo la karume ili kujipatia bidhaa zetu na Kwa mwaka tunapunguzo la bei Kwa asilimia 20 hivyo wake kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka Kampuni ya wa asili asilia ."amesema Munisi

Ameongeza kuwa anatambua kuwa kulikuwa na changaoto ya Ugonjwa wa Corona lakini kwasasa anamshukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri hivyo wananchi hususani wa mkoa wa Dar es Salaam wake kwenye maonyesho hayo kupata bidhaa mbalimbali.

Munis amesema kuwa baada ya kimalizika maonyesho Viwanja vya sabasaba wanapatikana Wilayani kinondoni ,eneo la salasala uwanja  wa Magofuni  jijini Dar es salaam. ambapo mawasiliano ni 0713222956.

Pia unaweza kutembelea kwenye mitandao ya kijamii ,Facebook Twitter ,na mengineyo Kama wa asili asilia.
 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Denan Munis akimuonesha moja ya bidhaa zake zilizopo kwenye banda hilo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...