Charles James, Michuzi TV
KATIKA kutimiza ahadi yake kwa Wananchi wa Wilaya ya Chemba, Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM), Mariam Ditopile amekabidhi msaada wa Mifuko 150 ya Saruji na Magodoro 30 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Makorongo.

Mifuko hiyo 150 ya Saruji itatumika kuendeleza ujenzi wa wa Shule Shikizi na Zahanati ya Kijiji cha Moto ambapo while hiyo itapokea mifuko 100 na zahanati hiyo ikipewa mifuko 50.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, Mbunge Ditopile amesema misaada hiyo ameitoa ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea maendeleo watanzania.

Ditopile amesema alifanya ziara kwenye Wilaya hiyo na kukutana na changamoto ya magodoro kwenye Shule ya Sekondari Makorongo na hivyo kuamua kuwaletea idadi hiyo ya magodoro ili iweze kuwasaidia.

" Ninafahamu kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania hasa wa kipato cha chini, hivyo kama Mbunge wa Vijana ni jukumu langu kuunga mkono serikali yetu katika kuwahudumia wananchi wetu.

Hivyo nikuombe Mhe DC upokee vifaa hivi tulivyovileta ili viweze kuwafikia wananchi wetu na viwe na manufaa kwao hasa kwa wanafunzi ambao kupitia magodoro haya sasa changamoto yao itakua imeisha lakini pia mifuko 100 ya saruji itaweza kumalizia ujenzi wa madarasa yanayojengwa," Amesema Mbunge Ditopile.

Kwa upande wake DC Odunga amempongeza Ditopile kwa uaminifu wake wa kutunza ahadi aliyowaadi wananchi wa Chemba kwa kuwaletea magodoro na mifuko hiyo ya Saruji.

" Nikupongeze sana Mhe Ditopile kwa moyo wako wa kuwakumbuka watu wetu wa Chemba, hii mifuko 150 ya Saruji ni mingi sana ni imani yetu kwamba itatusaidia sana kwenye ujenzi wa Zahanati na Shule zetu hasa hii Shikizi.

Ahadi yetu kwako ni moja tu kwamba msaada huu utawafikia wahusika ambao ni wananchi wa Chemba na wanafunzi wetu, Mkurugenzi wa Halmashauri nikutake usimamie hili vitu hivi viwafikie walengwa," Amesema DC Odunga.

Huu ni muendelezo wa kukamilisha ahadi zake unaofanywa na Mbunge Ditopile ndani ya Mkoa wa Dodoma ambapo wiki iliyopita alikabidhi magodoro na vitanda 20 kwa Shule ya Msingi Bereko yenye watoto wenye uhitaji lakini pia akisaidia ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari Dodoma pamoja na kuwanunulia Tenki la Maji.
 Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM), Mariam Ditopile akimkabidhi, Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma msaada wa Godoro kwa ajili ya Shule ya Sekondari Makorongo iliyopo wilayani humo.
 Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM, Mariam Ditopile akikabidhi mifuko ya Saruji kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule Shikizi na Zahanati ya Moto wilayani Chemba. Kulia ni DC wa Chemba, Simon Odunga.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo baada ya Ditopile kukabidhi mifuko 150 ya Saruji na Magodoro 30 wilayani hapo.
 Mifuko ya Saruji 150 na Magodoro 30 ambayo yametolewa na Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM, Mariam Ditopile kwa Wilaya ya Chemba kusaidia ujenzi wa Zahanati na Shule Shikizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...