WATOTO wote ni sawa! Hiyo ndio kauli ambayo Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM), Mariam Ditopile ameitoa wakati akikabidhi msaada wa vitanda 24 kwenye Shuye Msingi Beroke wilayani Kondoa, Dodoma inayohudumia pia watoto wenye mahitaji maalum.

Shule hiyo ya Msingi ina kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum ambacho kimejengwa na serikali ambapo Mbunge Ditopile amekabidhi Vitanda 24 na Magodoro yake vyenye thamani ya jumla ya Sh Milioni Sita.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mbunge Ditopile amewataka wazazi wenye watoto ambao wana mahitaji maalum kutowafungia ndani watoto wao badala yake wawapeleke shule kupata elimu kwani ni haki yao ya msingi.

Amesema kitendo cha watoto hao kufungiwa ndani na kukosa elimu kunawanyima fursa ya kushindwa kusoma na kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.

Ditopile amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli imekua ikiamini kuwa kila mwananchi ana haki sawa na mwingine bila kujali tofauti zao za Kidini, Kabila na Kimaumbile.

" Hawa watoto ni sawa na wengine, hakuna aliependa ila Mwenyezi Mungu ndie mwenye kuamaua atuumbaje sisi waja wake, hivyo tuwahudumie wenzetu bila ubaguzi wowote.

Nimeleta vitanda na magodoro haya 24 nikiamini yatasaidia kupunguza changamoto iliyokuepo kwa sababu tayari serikali imeshajenga kituo hiki sasa ni jukumu letu viongozi wengine kumsaidia Rais Magufuli katika kumalizia huduma zingine zinazotakiwa," Amesema Mbunge Ditopile.

Amewataka wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu kwani kupitia elimu ni rahisi kufikia uchumi wa kati unaotokana na viwanda ifikapo mwaka 2025.

" Najua kuna wazazi wanaofungia watoto wao ndani kwa sababu eti ni walemavu, hizo ni fikra dhaifu ambazo zimepitwa na wakati, binadamu wote ni sawa na tukiwapa elimu tutapata Mawaziri, Mabalozi na Wataalamu mbalimbali watakaokua msaada kwa Taifa," Amesema Ditopile.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Salum Myekah amemshukuru Mbunge huyo kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa utawafikia walengwa kama ambavyo imekusudiwa.

Myekah pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kutenga kiasi cha Sh Milioni 150 za kujenga kituo hiko na kuiomba Wizara ya Tamisemi kuwaongezea idadi ya walimu kwani wanao upungufu.

" Mbunge wetu tunakushukuru sana, umefanya jambo ambalo pia ni Sadaka kwa Mwenyezi Mungu, tunaomba usichoke kutusaidia na kushirikiana na sisi kila utakapojaliwa, na nikuahidi msaada huu utatumiwa na watoto wetu kama ulivyokusudiwa," Amesema Mwl Myekah.

Nae Mmoja wa watoto wenye uhitaji Juma Abdallah amemshukuru Rais Magufuli kwa kuruhusu masomo yaendelee huku pia akimpongeza Mbunge Ditopile kwa moyo wake wa kusaidia watanzania wenzake wenye uhitaji.

" Tunamshukuru Rais wetu kwa kuruhusu tuendelee na masomo, na wewe Mbunge pia asante kwa kutuletea magodoro haya, tunakuombea kwa Mungu siku nyingine utukumbuke na utuletee msaada mwingine," Amesema Juma.

 Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM), Mariam Ditopile (mwenye ushungi mweupe) akiwa na watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma kwenye Shule ya Msingi Bereko wilayani Kondoa, Dodoma na Viongozi wengine kata ya Beroke na Wazazi wakati akikabidhi Vitanda na Magodoro yake vipatao 24.
 Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM) Mariam Ditopile akizungumza na Viongozi, Wananchi na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bereko wakati alipofika shuleni hapo kukabidhi msaada wa Vitanda na Magodoro 24 kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma kwenye  Shule hiyo.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mariam Ditopile akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa Vitanda na Magodoro 24 kwenye Shule ya Msingi Bereko wilayani Kondoa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
 Vitanda na Magodoro 24 ambayo yametolewa na Mbunge wa Viti Maalum Vijana (CCM), Mariam Ditopile kwenye Shule ya Msingi Bereko wilayani Kondoa leo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.
 Baadhi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule ya Msingi Bereko wilayani Kondoa ambao wamepatiwa msaada wa Vitanda na Magodoro kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Vijana, Mariam Ditopile leo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...