Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu jana
akiwa ameongoza na Watumishi wa Shamba laMiti la Sao Hill akipewa
maelezo na Afisa Misitu, Glory Fortunatus wakati alipokuwa akitembelea
bustani ya miti ya shamva hilo lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na
Askari Wahifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mara alipowasili
katika makao makuu ya wilaya ya Mufindi kwa ajili ya ziaracya kikazi ya
siku moja katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo katika wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na
Askari Wahifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mara alipowasili
katika makao makuu ya wilaya ya Mufindi kwa ajili ya ziaracya kikazi ya
siku moja katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo katika wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa
Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi
wa Shamba la Miti la Sao Hill wakati alipofanya ziara ya kutembelea
bustani ya miti katika shamba hilo lilipo katika wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili,
Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongoza na baadhi ya Watumishi wa Shamba
la Miti Sao Hill wakati akikagua vifaa maaalum vya kuoteshea miti
kabla ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa.
Naibu
Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizunguma na Meneja wa
Shamba la Miti Sao Hill pamoja na Afisa Misitu Glory Fortunatus ( wa kwa
kushoto) wakati akiangalia miti iliyooteshwa kwa vifaa maalumu ambayo
ipo tayari kwa ajili ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa.
Naibu
Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizunguma na Meneja wa
Shamba la Miti Sao Hill pamoja na Afisa Misitu Glory Fortunatus ( wa kwa
kushoto) wakati akiangalia miti iliyooteshwa kwa vifaa maalumu ambayo
ipo tayari kwa ajili ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa.
( Picha zote na Wizara ya Malasili na Utalii)
************************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Constantine Kanyasu
ameonesha kusikitishwa na uwepo wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi
ya miaka 10 baina ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) ambazo zote ni Taasisi za Serikali
kuwa jambo hilo sio la kawaida.
Ameyasema hayo jana
wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Shamba la Miti la Sao Hill
linalosimamiwa na TFS lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Amesema eneo hilo la
ardhi lenye mgogoro lina ukubwa wa hekta 1705 ambazo kati ya hizo hekta
600 zilishapandwa miti na TFS ila baada ya mgogoro huo kuibuka kila
Taasisi ikidai kuwa eneo hilo ni lake ilipelekea TFS kushindwa kumalizia
kupanda miti katika eneo lililokuwa limebaki lenye jumla ya hekta 800.
Kufuatia hali hiyo,
Mhe. Kanyasu ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo
ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ishughulikie mgogoro huo uliopo baina ya
JKT Mafinga na Shamba la Miti Sao Hill ili kila Taasisi ijikite kwenye
majukumu yake ya msingi.
” Mgogoro huu
usipotafutiwa ufumbuzi wa haraka utaleta athari, Kitendo cha JKT Mafinga
kung’oa vigingi vilivyowekwa na TFS kwa ajili ya kubainisha mipaka
haileti picha nzuri ikizingatiwa kuwa zote hizo ni Taasisi za
Serikali” alisisitiza.
Amesema endapo Kamati
hiyo Ulinzi na Usalama itafika mwisho na kushindwa kupata majibu juu ya
mgogoro huo imshirikishe Mkuu wa mkoa wa Iringa ili mgogoro huo uweze
kuisha.
Amesema ni lazima
mgogoro huo ufike mwisho na ikishindikana Mkuu wa Mkoa ashirikishwe hali
itakayosaidia kuleta suluhu ya kudumu na kuzifanya Taasisi hizo
kuendelea kutoa huduma kwa jamii badala ya kuendelea kusigana kila
kukicha.
” Nina amini Mkuu wa mkoa ana vyombo na. uwezo wa kumaliza
mgogoro huu kwa vile hizi zote ni Taasisi za Serikali” alisisitiza
Mhe.Kanyasu
Hata hivyo,
Mhe.Kanyasu amesema endapo Mkuu wa Mkoa atashindwa kuutafutia majibu
mgogoro huo basi aitaarifu Wizara ya Maliasili na Utalii ili iweze
kukutana Wizara husika kwa lengo la kumaliza mgogoro huo.
Amesema anataka
mgogoro huo ufike mwisho na kama nyaraka zitaonesha kuwa eneo hilo la
JKT basi JKT wapewe na kama ikithibitika ni eneo hilo ni mali ya TFS
wapewe ili waweze kupanda miti.
” Jukumu letu sisi ni
kupanda miti tunachotaka ni kuona eneo hilo linapandwa miti bila
kujali kapanda nani JKT au TFS ” alisisitiza Mhe.Kanyasu.
Hata hivyo,
Mhe.Kanyasu amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuushughulikia mgogoro
huo licha ya kuwa umekuwa ukienda taratibu sana na hivyo kasi ya TFS
kumalizia kupanda miti katika eneo hilo imekuwa ikitatizwa na kuwepo kwa
mgogoro huo.
Kwa upande wake, Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Juma Mwita amesema mgogoro huo wa ardhi



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...