Na Said Mwishehe, Michuzi TV

 ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Nape Nnauye amesema chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli nchi yetu imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo na  amerudisha heshima ya utumishi umma huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwamba katika Uchaguz Mkuu mwaka huu Rais Magufuli atapewa tena miaka mitano ili aendelee kunyoosha mambo.

Nape amesema hayo leo Julai 3,2020 wakati anazungunza na wananchi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi alipokuwa akiwashukuru kwa kuwa pamoja kwa kipindi cha miaka mitano na wakati huo huo kuwaambia Julai 14,2020  anakwenda kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake(CCM) na imani yake atateuliwa,hivyo wananchi hao wamuunge mkono.

Wakati anazungumza kwenye mkutano wa hadhara Nape ametumia nafasi hiyo kuelezea maendeleo ambayo yamefanyika katika jimbo la Mtama chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.Magufuli akitolea mfano wa barabara ya lami kutoka Mtwara mpaka Masasi.

"Barabara kutoka Mtwara mpaka Masasi hii barabara yenu ni kwasababu Rais alibana matumizi, pia amerudisha heshima ya utumishi  na ndio maana mpaka leo unawasikia watumishi wa wanalalama vyuma vimekaza ,unajua maana yake nini hakuna semina,hakuna posho za hovyo hovyo.

"Na sisi tunajua maendeleo yoyote yanamaumivu yake ,unataka uvune vizuri amka asubuhi nenda kalime ,utaumia kwa muda lakini utakapopeleka magunia 100 gulioni unaanza kula maisha , sasa kuna watu wanataka wasiumie lakini wale maisha haiwezekani, dunia haiko hivyo.

"Ndio maana wana Mtama niwahakikishieni,tutampa tena Rais Magufuli miaka mitano amalizie kazi ya kunyoosha mambo, akishakamilisha tutakwenda na ndio utaratibu wa nchi yetu, alianza Mwalimu Nyerere akanyoosha nyoosha, akaja Mzee ruksa akalegeza kidogo, akaja Mkapa ukapa ukasambaa kila mahali akakaza kidogo, akaja Jakaya Kikwete akalegeza , amekuja Mzee wetu wa Hapa Kazi Tu amekaza kidogo, baada ya hapo atakuja mwingine sijui Nape,atalegeza kidogo ,mambo yatakwenda mbele.

" Mimi naamini mmenielewa ,nisema sana naomba mnisamehe lakini nilidhani niguse mambo Mtama yetu sasa hivi njema hebu haya mavyama tuwekeni pembeni ,hakuna hata chama kimoja kimezaliwa hapa tusigombane kwasababu ya vyama ,Mtama inapendeza tukikawa wenyewe, inapendeza,tufurahi tuijenge Mtama yetu,"amesema Nape.

Hata hivyo amewaambia wananchi wa Jimbo la Mtama kuwa "Nimekuja kuwashukuru kwa kuishi nanyi kwa kipindi cha miaka mitano,na nimekuja kuwaambieni Julai 14 ,2020 naenda kuchukua fomu kwenye Chama changu,ndani ya Chama changu sina mashaka nitashinda lakini baada ya kuteuliwa na chama changu naomba mniunge mkono tena  tukamilishe kazi tuliyoianza.

"Tumlee mtoto wetu anaitwa Halmashauri, tukamilishe umeme kule kulikobaki, tupeleke huduma za afya kule ambako hazijafika, tuioboreshe Mtama yetu ,mimi na nyie tukifanya kazi pamoja inawezekana ,amueni kwa pamoja,tusonge mbele kwa pamoja."

 ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Nape Nnauye

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...